IKUNGI: MKUU WA WILAYA YA IKUNGI Mhe. MIRAJI MTATURU AMEONGOZA MAZISHI YA MGONTO DIWANI WA KATA YA SIUYU

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Jumanne Mtaturu ameongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekua DIWANI wa Kata ya Siuyu iliyoko Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu Akihutubia umati wa waombolezaji kwa kuwapa pole kwa msiba, na kuwaasa kuwa na uvumilivu kwa kipindi hichi kigumu kwani hakuna ambaye hajaguswa na msiba huu na Serikali Iliupokea kwa masikitiko makubwa na hakuna la kufanya zaidi ya kumuombea mwenzetu ili Mungu ampe pumziko la Milele.

Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na wilaya jirani za mkoa wa Singida wakisubiri kuuaga mwili wa marehemu Mhe. Mgonto.


Umati wa wananchi walioshiriki Mazishi ya Marehemu Mhe. Mgonto. Nyumbani kwake Siuyu Wialayani Ikungi Singida.

Viongozi wa Chama na Serikali wakiwa wamekaa kwa huzuni kubwa wakisubiri kuuaga Mwili wa Marehemu Mhe. Mgonto nyumbani kwake Siuyu wilayani Ikungi Singida.

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Ikungi Mhe. Ally Juma Mwanga. akitoa salam za pole kwa wafiwa na waombolezaji kwa msiba mzito uliowakuta wa Marehemu Mhe. Mgonto. 

"Tulipo pata taarifa ya msiba sisi kama Halmashauri tuliipokea taarifa kwa masikitiko makubwa kweli ila niwaombe tuendelee kuwa na umumilivu kwani msiba huu ni mkubwa na ni mzito.

Aidha Mhe. Ally Mwanga Amewaasa Waheshimiwa Madiwani kuwa na uvumilivu na kumuombea Mwenzao na kuendeleza yale ya maendeleo aliyoyaacha katani kwake na has a Miradi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Mhe. Mika Likapaka Akitoa salam za pole kwa Familia, wafiwa na kwa Chama. 

"Kwa Masikitiko makubwa kabisa Sisi Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi tumeupokea msiba huu kwa maumivu makubwa na kwa majonzi yasiyo elezeka kwani Mhe Mgonto Amerudisha heshima ya Chama Cha Mapinduzi Kata ya Siuyu kwakweli Nakosa haata niseme nini".

Alimaliza kwa kusema Chama Kitakua karibu na familia hivyo ni kuendelea kumuombea Marehemu ili Mungu ampe pumziko la Milele.

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Ndg Solomon Kasaba akitoa salam za pole kwa wafiwa wote kwa msiba mkubwa ulotokea wa Marehemu Mhe. Mgonto Diwani wa Kata ya Siuyu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Lawrence Kijazi akiwa amesimama kwa unyenyekevu na kwa masikitiko makubwa kuondokewa na Diwani makini katika kutoa mchango wa maendeleo katika Halmashauri yake.

Waombolezaji na Waheshimiwa Madiwani wakishusha Jeneza kumzika Mhe.Ramadhani Mgonto.

Hii ndiyo Safari ya MWISHO ya Mpendwa wetu Mhe.Ramadhani Mgonto. Aliyekua Diwani wa Kata ya Siuyu. 

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE.

MWISHO.


Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida