Posts

Showing posts from September, 2022

WAZEE IKUNGI WAKUTANA NA DC MURO

Image
Na Mathew Anton Singida. Ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya siku ya wazee Duniani ambayo kimkoa maadhimisho yatafanyika katika Wilaya ya Ikungi, baadhi ya wazee wamekutana na Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry Muro ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho yatakayifanyika kesho tarehe 01/10/2022 Wakizungumza ofisini kwa Dc Muro wazee hao wameishukuru serikali ya wilaya kwa namna inavyoshughulikia kero na changamoto zinazowakumba wazee na kumuhakikisha Dc Muro kuwa kesho wana jambo la kusema kwa Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan Katika mazungumzo hayo Dc Muro amewahakikisha wazee kuwa serikali itaendelea kuondoa kero na changamoto zinazowakumba wazee ikiwemo kuweka mfumo endelevu wa kuhakikisha mabaraza ya wazee kuanzia ngazi ya wilaya, kata na vijijini yanafanya kazi ipasavyo hatua itakayowawezesha wazee wenyewe kutatua changamoto ndogondogo zinazowakabili wakati serikali ikiendelea kutatua kero mtambuka za wazee.

ASKOFU AFARIKI DUNIA AKIHUBIRI IBADA YA MAZISHI MKOANI TAANGA

Image
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa George Chiteto amefariki dunia jana mchana mara baada ya kumaliza kuhubiri katika mazishi ya mke wa Askofu Lugendo wa Dayosisi ya Mbeya Bi. Hilda Lugendo yaliyofanyika wilayani Muheza mkoani Tanga. Tukio hilo la huzuni limekuja ghafla mara baada ya kumaliza mahubiri katika msiba huo, Askofu George Chiteto alirudi kukaa kwenye kiti ili taratibu zingine za ibada ziendelee, alianza kujisikia vibaya, akaishiwa nguvu kisha kupoteza fahamu. Utaratibu wa kumkimbiza hospitali ulifanyika haraka na kufikishwa katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza Tanga na saa chache akaaga dunia. Askofu George aliwekwa wakfu Jumapili iliyopita Agosti 28, 2022 kuwa Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa iliyopo wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma na Septemba 03, 2022 akawa ameaga dunia akihudumu nafasi hiyo ya uaskofu wa Dayosisi hiyo kwa takribani siku kati ya tano tu. Askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, aliyekuwepo katika ibada hiyo ya mazis