Posts

Showing posts from August, 2021

JIMBO LA SINGIDA MAGHARIBI LAPATIWA MILIONI 140 KUTEKELEZA MIRADI YA ELIMU

Image
Napenda kuwataarifu Wananchi wa Jimbo la Singida Magharibi wote na walipa kodi kuwa Jimbo latu Tumepewa pesa Milioni 140 Yaani Tshs 140,000,000 kutoka TEA kwa ajili ya 1. Kujenga Matundu 24 ya vyoo Mtunduru shule ya msingi Tshs 40,000,000 2. Kujenga Madarasa 3 Mtunduru Shule ya Msingi Tshs Milioni 60. yaani Tshs 60,000,000 3. Kujenga vyoo vya Matundu 24. Ilolo Shule ya Msingi Tshs Millioni 40 yaani 40,000,000 Asante Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan. Asante sana TEA Asante Mungu. Mungu Ibariki Tanzania Tutashauri miradi hii yote itekelezwe kwa Forced account Jumla Tshs 140,000,000 Kesho Mbunge wenu nitafanya ziara maeneo Haya yote kuwapa ujumbe wanancnhi wajue pesa hizi ili wawe makini katika kusimamia na Board za shule Elibariki Immanuel Kingu Mbunge Singida Magharibi #SingidaMagharibi #MaendeleoKwanza

MAKAMANDA WA CHADEMA SINGIDA MASHARIKI WATIMKIA CCM

Image
WANACHAMA wawili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wa Jimbo la Singida Mashariki Katika Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida wamekihama Chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na kile walichodai kukosekana kwa Demokrasia halisi wanayoinadi viongozi wakuu wa Chama hicho kila kukicha. Wanachama hao ni aliyekuwa kampeni meneja wa kata ya Unyahati Philemon Ghula na aliyekuwa Mgombea Udiwani Kata ya Makiungu Julius Sunna. Akizungumza mara baada ya uamuzi huo Ndugu Philemon Ghula amesema wamechukua uamuzi huo ili kuunga mkono juhudi za Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu kwa kazi nzuri wanayoifanya. " Rais Samia anafanya kazi nzuri sana inayoonekana na kila mmoja wetu, lakini pia Mbunge wetu Mhe. Mtaturu anatutumikia wananchi na tofauti ya yeye na mtangulizi wake inaonekana dhahiri, hivyo hatuoni sababu ya kutowaunga mkono, " alisema Ghula. Nae Sunna amesema amechukua uamuzi huo kutokana na kuchoshwa na ub