Posts

Showing posts from November, 2021

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

Image
Na Musa Njoghomi Sehemu ya Kwanza. Ikweta(Equator) ni mstari unaoigawa dunia katikati na kutoa pande kuu mbili zinazolingana, ambazo ni ukanda wa kaskazini na ukanda wa kusini(Northern & Southern hemisphere) Kijiografia maeneo ya ukanda wa *Ikweta* ndio maeneo pekee yenye sifa za mvua nyingi,ardhi yenye rutuba & misitu mikubwa na ya kijani( Evergreen forest) hii ni kwasababu ya hali ya hewa inayopatikana katika ukanda huu( high temperature) with high evaporations. Kwetu sisi Tanzania mstari wa Ikweta umepita jirani yetu hapo nchini Kenya, hivyo tulipaswa kuwa na misitu mingi sana mithili ya Congo Forest. Nchi zilizopo Northern Pollar & Souther pollar haziwezi kuwa na miti mingi kwasababu ya nature ya hali ya hewa. Nchi za pollar regions huona jua kwa nadra sana sio sawa na sisi. hivyo wao kuwa misitu mingi kama sisi ni changamoto. Pia wanachangamoto za barafu eg, nchi kama Iceland,Newzealand etc Sisi tuliopo Ikweta/ Karibu na Ikweta ndio tunapaswa kuwa na wajibu wakukabili

CHIFU SINGU MISSANGA ASIMIKWA KUWA KIONGOZI WA KABILA LA WANYATURU

Image
Na: Chifu Ahmed Missanga. Leo Tarehe 17/11/2021 imekuwa baraka Ihanja Wilayani Ikungi Mkoani Singida Amesimikwa rasmi Chifu Singu Missanga Senge Kuwa kiongozi wa Utemi wa UNYIKUNGU katika kabila la Wanyanturu. Hafla hii ya usimikwaji ilianza kwa Dua Maalum ilioyo ongozwa na Viongozi wa Dini Shekhe, Mchungaji na Viongozi wa Kimila ya Kknyaturu. Chifu Singu Missanga amesimikwa na Baraza la Wazee la ukoo wa Chifu Missanga Senge katika kabila la Wanyaturu na kushuhudiwa na Chifu Mkuu wa Ikungi Abraham Gwau. Akimwakilisha Jerry Muro Mkuu wa wilaya wa Ikungi, Katibu Tawala Wilaya Ndg. Dijovison Ntangeki amesisitiza Viongozi wa Kimila kuwa ndio nguzo ya Amani na uwajibikaji hivyo watumie nafasi hizo kusaidia kuelelimisha jamii kuacha Mila potofu, kuhamasisha  jamii kuenzi mila na tamaduni za Tanzania. Ikiwemo uhamasishaji  upendo, maridhiano, umoja na mshikamano wa taifa ikienda sambamba na kulingania tunu za taifa pamoja na upendo ili kuondoa ukiukwaji wa Hali za binadamu wenye vionjo vya ub

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR Mhe. HEMEDI SULEIMAN ABDULLA AIPONGEZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE INAYOSHUGHULIKIA MAGONJWA

Image
Na: Kassim Abdi - Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza Kamati ya kudumu ya Bunge inayoshughulikia masuala ya Ukimwi, Kifua kikuu, Madawa ya kulevya pamoja na maradhi yasioambukiza kwa ushirikiano wake kwa serikali ya mapinduzi Zanzibar. Mhe. Hemed alieleza hayo katika kikao maalum kilichowakutanisha wajumbe wa kamati hiyo waliofika afisini kwake vuga jijini Zanzibar kwa lengo la kubadilishana nae mawazo. Alieleza kuwa, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inafarijika kutokana na ushirikiano wanaoupata kutoka kwa kamati hiyo, kwa ushirikiano wa pamoja na viongozi wake ambapo kwa kiasi kikubwa imesaidia kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya. Alibainisha kwamba, kutokana na Zanzibar kuwa nchi ya visiwa, imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya upitishaji wa madawa ya kulevya, kutokana na uwepo wa bandari nyingi zisizokuwa rasmi, zinazotumiwa na wahalifu wa vitendo hivyo. Aidha, Makamu wa Pili wa Rais alisema kutokana na kadhia hiyo ya uwingizwaji

KENAN AKISHUKURU CHAMA CHA MAPINDUZI

Image
Kenan L. Kihongosi KATIBU MKUU UVCCM : Kwanza namshukuru MWENYEZI MUNGU kwa uzima na Afya njema. Pili nakishukuru Chama Cha Mapinduzi sambamba na Mweyekiti wake ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mheshimiwa SAMIA SULUHU HASSAN Ambaye dhahiri ametukopesha imani kubwa nasi UVCCM hatuna budi kumlipa Imani. Pia namshukuru katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo ambaye ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi kwa Uongozi wake mahiri na kutuongoza vyema sisi kama jumuiya ya vijana Tunasema Asante sana na tutazidi kufanya kazi kwa bidii zaidi. Pia Nawashukuru Wajumbe wote wa Sekretarieti kwa Ushirikiano Mkubwa na Mzuri katika kuimarisha ujenzi wa Chama Cha Mapinduzi. Hakika kitendo cha Chama cha Mapinduzi kuteua watendaji wa UVCCM wengi kwa wakati mmoja Kuwa watendaji wa CHAMA kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa hii imeongeza ARI Kubwa kwa vijana na kwa Watendaji wenzangu. Hakika Chama Cha Mapinduzi Chini ya Mweyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano

WADAU KUWEKEZA KWENYE KILIMO CHA ALIZETI IKUNGI

Image
S erikali ya Wilaya ya Ikungi imefanikiwa kuwaunganisha wadau wenye nia ya kuwekeza Katika Sekta ya kilimo cha alizeti na Taasisi za kifedha ikiwemo Benki ya Maendeleo ya kilimo Hatua hiyo imekuja baada ya kumalizika kwa kikao maalum cha majadiliano ya mwisho ya namna ya kuwawezesha wadau waliochukua mashamba yenye ukubwa wa hekari 4,500 kwa ajili ya Kuwekeza kwenye kilimo cha alizeti Tayari serikali imewezesha kuundwa kwa kikosi kazi * (task force * ) inayojumuisha wadau wanaolima zao la alizeti, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kupitia afisa kilimo na afisa ardhi , pamoja na taasisi zote za kifedha zikiwemo benki za bishara kwa Pamoja zimekubalia kuungana kwa ajili ya kutatua changamoto zilizojitokeza. Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Jerry Muro Amewashukuru Wadau hao kwa Kuunga mkono juhudi hizo na kuahidi kutoa ushirikiano. *Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ikungi * * 01/11/2021 *