IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

Na Musa Njoghomi
Sehemu ya Kwanza.

Ikweta(Equator) ni mstari unaoigawa dunia katikati na kutoa pande kuu mbili zinazolingana, ambazo ni ukanda wa kaskazini na ukanda wa kusini(Northern & Southern hemisphere)

Kijiografia maeneo ya ukanda wa *Ikweta* ndio maeneo pekee yenye sifa za mvua nyingi,ardhi yenye rutuba & misitu mikubwa na ya kijani( Evergreen forest) hii ni kwasababu ya hali ya hewa inayopatikana katika ukanda huu( high temperature) with high evaporations.

Kwetu sisi Tanzania mstari wa Ikweta umepita jirani yetu hapo nchini Kenya, hivyo tulipaswa kuwa na misitu mingi sana mithili ya Congo Forest.

Nchi zilizopo Northern Pollar & Souther pollar haziwezi kuwa na miti mingi kwasababu ya nature ya hali ya hewa. Nchi za pollar regions huona jua kwa nadra sana sio sawa na sisi. hivyo wao kuwa misitu mingi kama sisi ni changamoto. Pia wanachangamoto za barafu eg, nchi kama Iceland,Newzealand etc

Sisi tuliopo Ikweta/ Karibu na Ikweta ndio tunapaswa kuwa na wajibu wakukabili mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kupanda miti mingi,Kupunguza ukataji miti kiholela ili kupunguza joto duniani. Pia nchi zilizoendelea kupunguza matumizi ya nishati zinazotoa moshi  unaoenda kutoboa Ozone Layer hivyo kupelekea miale ya jua kuja moja kwa moja katika uso wa dunia na kusababisa joto kubwa(Global warming)


TUPANDE MITI KWA WINGI KWA FAIDA YETU NA DUNIA.

#musanjoghomi
#bazotvnews
#bazotvonline

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida