Posts

Showing posts from April, 2020

SHANTA MINING COMPANY LTD YAIKABIDHI WILAYA YA IKUNGI VIFAA VYA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA VYENYE THAMANI YA. 2.2 MILIONI

Image
   Na Bazil Mjungu: Ikungi - Singida Kampuni ya Uchimbaji Madini - Shanta Mining Company Limited ya Mkoani Singida, Imemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi msaada wa Vifaa vya Kujikinga na Virusi vya Corona vyenye Thamani zaidi ya Milioni 2.2 kuunga mkono juhudi za Mhe Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha ugonjwa wa Corona hauenei Nchini.   Akikabidhi msaada huo,  kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,  Ndug Justice Lawrence Kijazi,  jana April 24 / 2020 kwa niaba ya Kampuni hiyo Eng. Philbert Rweyemamu Meneja Mkuu,  Meneja huyo amesema kampuni yao imetoa msaada huo wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona,  ikiwa ni kushiriki moja kwa moja kwa vitendo ili kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli. Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Eng. Philbert Rweyemamu amesema pamoja na vifaa hivyo walivyotoa,  Kampuni ya Shanta Mining Limited Imekabidhi hivi karibuni Tsh Milioni 100 kwenye m