Posts

Showing posts from 2021

TANZANIA IKO MIKONONI MWA MUNGU: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

Image
Na: Bazil Mjungu - Lindi. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Tanzania iko mikononi mwa Mungu na ndiyo maana imeendelea kuwa nchi yenye amani na utulivu na kimbilio la mataifa yaliyopoteza tumaini. “Nchi hii imeshikwa na Mwenyezi Mungu na ni kwa sababu viongozi wa dini wanaendelea kuliombea Taifa hili, kwa hiyo na sisi tunalo jukumu la kuhakikisha kwamba nchi hii inabaki kwa salama,” Waziri Mkuu. Mhe. Majaliwa Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Desemba 31, 2021) wakati akizungumza na waumini baada ya kushiriki ibada ya Ijumaa na kuzindua msikiti wa Nkowe, ulioko kata ya Nkowe, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi. Amesema Serikali zote tangu awamu ya kwanza hadi ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, zimeendeela kuheshimu uwepo wa dini nchini kwani miongozo na mafundisho yanayotolewa na viongozi wa dini mbalimbali yanawafanya waumini wao kuwa raia wema. “ Mheshimiwa Rais alipoingia madarakani alikutana na Mababa Askofu wote

MTATURU JIMBO CUP YAHITIMISHWA RASMI NA WAZIRI WA SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO MHE. INNOCENT BASHUNGWA

Image
Na Bazil Mjungu Singida: Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe Innocent Bashungwa leo Tarehe 26/12/2021 Amehitimisha Rasmi Mashindano ya Mpira wa Miguu yaliyojulikana Kama Mtaturu Jimbo Cup Katika Uwanja wa Sekondari Ikungi, Katika Jimbo la Singida Mashariki Wilayani Ikungi, Ambapo Katika Kuhitkmisha ligi hiyo kulikua na Mechi ya Fainali iliyohusisha timu ya Mampando Fc na Matongo Fc ambambo mechi iliisha kwa Dakika 90 kwa Timu ya Matongo Fc kuibuka dhidi ya Mampando Fc. Waziri Bashungwa ameonyesha kufurahishwa na Taarifa ya Mashindano hayo na kumpongeza mdhamini wa ligi hiyo Mhe. Miraji Mtaturu kwa jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo Jimboni humo. " Kipekee niseme tu niwe mshuhuda hata Bungeni Mhe. Mtaturu amekua akijenga hoja zenye masilahi kwa wananchi wake na hata akiomba Mradi unaohusu Jimbo Basi ukiwa Waziri wa Wizara aliyoomba Jambo utamuona akifuatilia Hatua zote ili Kuhakikisha alichokiomba kinawafikia Wananchi wake" Alisema Mhe. Bashungwa Aidha, Mhe. B

MTATURU ACHANGIA VYEREHEANI 10 CHUO CHA KIISLAM - JIMBONI

Image
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu ameshiriki Sherehe za Maadhimisho ya kutimiza Mwaka Mmoja tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Kiislamu Cha (Almadrasatul Tah Dhiibul Islaamiyaa) kilichopo Kata ya Dung'unyi Wilayani Ikungi Singida Ambapo amewaomba Viongozi wa Dini kuhubiri Umoja na mshikamano. Mbungehuyo baada ya kuwasili na kujionea Mazingira ya Wanafunzi wanayojifunzia alionyesha kufurahishwa na usimamizi wa Chuo hicho ambapo bila kumumunya maneno aliamua kutamka kuchangia Vyerehani 10 na Seti moja ya Ufundi Seremala ili kuwafanya Wanafunzi kusoma kwa vitendo na wakimaliza masomo yao wakawe mfano Bora kwa familia zao. Akizungumza Katika Hafla hiyo ya Maadhisho Mhe. Mtaturu akasema Nimefurahishwasana na mafunzo haya mnayofundishwa hapa Vijana,  na Ninataka niwaambieni kila mtu anapaswa kujua wakati upi wa kujiandaa kimasomo na wakati upi wa kupoteza, na Ninataka niwahimize wazazi na walezi wa hawa Wanafunzi hakuna kitu kizuri Kama kumuunga mkono mtoto ukigundua an

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

Image
Na Musa Njoghomi Sehemu ya Kwanza. Ikweta(Equator) ni mstari unaoigawa dunia katikati na kutoa pande kuu mbili zinazolingana, ambazo ni ukanda wa kaskazini na ukanda wa kusini(Northern & Southern hemisphere) Kijiografia maeneo ya ukanda wa *Ikweta* ndio maeneo pekee yenye sifa za mvua nyingi,ardhi yenye rutuba & misitu mikubwa na ya kijani( Evergreen forest) hii ni kwasababu ya hali ya hewa inayopatikana katika ukanda huu( high temperature) with high evaporations. Kwetu sisi Tanzania mstari wa Ikweta umepita jirani yetu hapo nchini Kenya, hivyo tulipaswa kuwa na misitu mingi sana mithili ya Congo Forest. Nchi zilizopo Northern Pollar & Souther pollar haziwezi kuwa na miti mingi kwasababu ya nature ya hali ya hewa. Nchi za pollar regions huona jua kwa nadra sana sio sawa na sisi. hivyo wao kuwa misitu mingi kama sisi ni changamoto. Pia wanachangamoto za barafu eg, nchi kama Iceland,Newzealand etc Sisi tuliopo Ikweta/ Karibu na Ikweta ndio tunapaswa kuwa na wajibu wakukabili

CHIFU SINGU MISSANGA ASIMIKWA KUWA KIONGOZI WA KABILA LA WANYATURU

Image
Na: Chifu Ahmed Missanga. Leo Tarehe 17/11/2021 imekuwa baraka Ihanja Wilayani Ikungi Mkoani Singida Amesimikwa rasmi Chifu Singu Missanga Senge Kuwa kiongozi wa Utemi wa UNYIKUNGU katika kabila la Wanyanturu. Hafla hii ya usimikwaji ilianza kwa Dua Maalum ilioyo ongozwa na Viongozi wa Dini Shekhe, Mchungaji na Viongozi wa Kimila ya Kknyaturu. Chifu Singu Missanga amesimikwa na Baraza la Wazee la ukoo wa Chifu Missanga Senge katika kabila la Wanyaturu na kushuhudiwa na Chifu Mkuu wa Ikungi Abraham Gwau. Akimwakilisha Jerry Muro Mkuu wa wilaya wa Ikungi, Katibu Tawala Wilaya Ndg. Dijovison Ntangeki amesisitiza Viongozi wa Kimila kuwa ndio nguzo ya Amani na uwajibikaji hivyo watumie nafasi hizo kusaidia kuelelimisha jamii kuacha Mila potofu, kuhamasisha  jamii kuenzi mila na tamaduni za Tanzania. Ikiwemo uhamasishaji  upendo, maridhiano, umoja na mshikamano wa taifa ikienda sambamba na kulingania tunu za taifa pamoja na upendo ili kuondoa ukiukwaji wa Hali za binadamu wenye vionjo vya ub

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR Mhe. HEMEDI SULEIMAN ABDULLA AIPONGEZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE INAYOSHUGHULIKIA MAGONJWA

Image
Na: Kassim Abdi - Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza Kamati ya kudumu ya Bunge inayoshughulikia masuala ya Ukimwi, Kifua kikuu, Madawa ya kulevya pamoja na maradhi yasioambukiza kwa ushirikiano wake kwa serikali ya mapinduzi Zanzibar. Mhe. Hemed alieleza hayo katika kikao maalum kilichowakutanisha wajumbe wa kamati hiyo waliofika afisini kwake vuga jijini Zanzibar kwa lengo la kubadilishana nae mawazo. Alieleza kuwa, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inafarijika kutokana na ushirikiano wanaoupata kutoka kwa kamati hiyo, kwa ushirikiano wa pamoja na viongozi wake ambapo kwa kiasi kikubwa imesaidia kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya. Alibainisha kwamba, kutokana na Zanzibar kuwa nchi ya visiwa, imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya upitishaji wa madawa ya kulevya, kutokana na uwepo wa bandari nyingi zisizokuwa rasmi, zinazotumiwa na wahalifu wa vitendo hivyo. Aidha, Makamu wa Pili wa Rais alisema kutokana na kadhia hiyo ya uwingizwaji

KENAN AKISHUKURU CHAMA CHA MAPINDUZI

Image
Kenan L. Kihongosi KATIBU MKUU UVCCM : Kwanza namshukuru MWENYEZI MUNGU kwa uzima na Afya njema. Pili nakishukuru Chama Cha Mapinduzi sambamba na Mweyekiti wake ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mheshimiwa SAMIA SULUHU HASSAN Ambaye dhahiri ametukopesha imani kubwa nasi UVCCM hatuna budi kumlipa Imani. Pia namshukuru katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo ambaye ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi kwa Uongozi wake mahiri na kutuongoza vyema sisi kama jumuiya ya vijana Tunasema Asante sana na tutazidi kufanya kazi kwa bidii zaidi. Pia Nawashukuru Wajumbe wote wa Sekretarieti kwa Ushirikiano Mkubwa na Mzuri katika kuimarisha ujenzi wa Chama Cha Mapinduzi. Hakika kitendo cha Chama cha Mapinduzi kuteua watendaji wa UVCCM wengi kwa wakati mmoja Kuwa watendaji wa CHAMA kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa hii imeongeza ARI Kubwa kwa vijana na kwa Watendaji wenzangu. Hakika Chama Cha Mapinduzi Chini ya Mweyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano

WADAU KUWEKEZA KWENYE KILIMO CHA ALIZETI IKUNGI

Image
S erikali ya Wilaya ya Ikungi imefanikiwa kuwaunganisha wadau wenye nia ya kuwekeza Katika Sekta ya kilimo cha alizeti na Taasisi za kifedha ikiwemo Benki ya Maendeleo ya kilimo Hatua hiyo imekuja baada ya kumalizika kwa kikao maalum cha majadiliano ya mwisho ya namna ya kuwawezesha wadau waliochukua mashamba yenye ukubwa wa hekari 4,500 kwa ajili ya Kuwekeza kwenye kilimo cha alizeti Tayari serikali imewezesha kuundwa kwa kikosi kazi * (task force * ) inayojumuisha wadau wanaolima zao la alizeti, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kupitia afisa kilimo na afisa ardhi , pamoja na taasisi zote za kifedha zikiwemo benki za bishara kwa Pamoja zimekubalia kuungana kwa ajili ya kutatua changamoto zilizojitokeza. Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Jerry Muro Amewashukuru Wadau hao kwa Kuunga mkono juhudi hizo na kuahidi kutoa ushirikiano. *Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ikungi * * 01/11/2021 *

MAVUNDE AKABIDHI TV NA KING'AMUZI SHULE YA SEKONDARI MPUNGUZI

Image
Na Bazil Mjungu Dodoma: Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde leo Tarehe 29 October 2021 Amezungumza na wanafaunzi wa Shule ya Sekondari Mpunguzi na kuwapatia mrejesho wa Huduma zinazo letwa na Serikali  ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Mara baada ya Mazungumzo mazuri na Wanafunzi hao Mbunge huyo amewakabidhi Televisheni na King’amuzi cha Azam vyote vyeye Thamani ya Shilingi 1,745,000 kwa lengo la kuwapa Nafasi ya kujifunza zaidi na kupata habari mbalimbali za Nchi na za Kimataifa Pamoja  na kufuatilia kwa karibu Utendaji kazi wa Viongozi wa Serikali walio wachagua. Aidha, Mhe. Mavunde ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa madarasa 6 shuleni hapo yenye thamani ya Shilingi 120,000,000 na yeye kuahidi kuzisimamia kwa karibu na kikamilifu ili zilete matokeo yaliyokusudiwa. #antonymavunde #ssh #ikulutanzania #bazotvnews #bazotvonline #kaziiendelee #a

UFUNGUZI KIKAO CHA UWEKEZAJI WILAYA YA IKUNGI KILIMO CHA ALIZETI CHAPEWA KIPAUMBELE

Image
Na Bazil Mjungu Singida: Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Jerry Muro leo Tarehe 29 October 2021 amefungua kikao Cha Uwekezaji Katika sekita ya Kilimo Wilaya ya Ikungi. Katika kikao hicho Kaimu Mkuu wa Mkoa amesema uwekezaji katika kilimo wao wameona Ni vema kuanza na Uwekezaji wa Kilimo cha zao la Alizeti. Pamoja na Mambo mengine Kaimu Mkuu wa mkoa wa Singida Jerry Murro amesema halmashauri ya Wilaya ya Ikungi imetenga ekari zaidi ya laki Moja kwa ajili ya kilimo cha alizeti. Aidha Mhe Jerry Muro amesema tayari Wizara ya kilimo imeshatoa Mbegu bora za kilimo kiasi cha tani elfu 13 kwa ajili ya wakulima wa alizeti Wilayani Ikungi. Wajumbe wa  Kikao cha Uwekezaji Wakisikiliza Hotuba ya kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Jerry Muro. Ras Mstaafu Alhaji Salum Chima kushoto na Mkurugenzi wa JMC Eng. Msafiri wakisikiliza Hotuba ya Ufunguzi wa Kikao cha Uwekezaji. Wadau wa Kilimo wakisikiliza Hotuba ya Ufunguzi wa Kikao cha Uwekezaji iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Jerry Muro.

MHE. ANTONY MAVUNDE KUFANIKISHA UJENZI WA UZIO SHULE YA SEKONDARI DODOMA

Image
Na Bazil Mjungu Dodoma: Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini   Mhe. Anthony Mavunde ameahidi kufanikisha Ujenzi wa Uzio wa Shule ya Sekondari Dodoma kwa lengo la kuongeza Ulinzi kwa wanafunzi na mali za shule hiyo. Mbunge Mavunde ameyasema hayo leo Tarehe 29 October 2021 wakati wa hafla ya Mahafali ya kidato cha IV shuleni hapo kufuatia maombi yaliyowasilishwa na wanafunzi kupitia Risala iliyosomwa mbele yake. Mhe Mavunde amesema Atahakikisha analifanyia kazi swala hilo ikiwa ni yeye Mbunge na kwa kushirikiana na Wadau wa Elimu Lazima Miundombinu ya Shule zote Katika Jimbo la Dodoma Mjini zinakua zinaridhisha wakati wote. “ Nataka niwahakikishie Wanafunzi, Walimu na Wazazi kwamba tutamalizia ujenzi wa eneo la uzio lililobaki ili kulizungushia eneo lote la shule na uzio kwa madhumuni ya usalama wa wanafunzi na mali zote zilizopo shuleni tunashukuru kazi kubwa iliyofanywa na wanafunzi waliosoma hapa wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndg. Masanja Kadogosa kwa ujenzi wa uzio kwa awamu ya kw

SERIKALI YATENGA SH. BILIONI 170 UJENZI MKONGO WA TAIFA

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imetenga shilingi bilioni 170 kwa ajili ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa katika mwaka wa fedha 2021/2022. “Lengo letu ni kuwawezesha watoa huduma za mawasiliano kutumia miundombinu hii kuboresha huduma za mawasiliano nchini na kurahisisha ufikishwaji wa intaneti kwenye ofisi mbalimbali za sekta ya umma na binafsi” Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Oktoba 22, 2021) wakati alipofungua Mkutano wa Tano wa Mwaka wa TEHAMA Tanzania uliofanyika katika katika ukumbi wa mikutano wa AICC, jijini Arusha. Amesema fedha hizo zitawezesha kujenga kilomita 4,244 za Mkongo ili kufikisha jumla ya kilomita 12,563. Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuiagiza Wizara ya Habari, Sayansi na Teknolojia ya Habari isimamie kwa karibu mradi wa upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili wananchi wengi zaidi washiriki katika ujenzi wa uchumi wa kidijitali. “Hivi