MTATURU JIMBO CUP YAHITIMISHWA RASMI NA WAZIRI WA SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO MHE. INNOCENT BASHUNGWA
Na Bazil Mjungu Singida:
Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe Innocent Bashungwa leo Tarehe 26/12/2021 Amehitimisha Rasmi Mashindano ya Mpira wa Miguu yaliyojulikana Kama Mtaturu Jimbo Cup Katika Uwanja wa Sekondari Ikungi, Katika Jimbo la Singida Mashariki Wilayani Ikungi, Ambapo Katika Kuhitkmisha ligi hiyo kulikua na Mechi ya Fainali iliyohusisha timu ya Mampando Fc na Matongo Fc ambambo mechi iliisha kwa Dakika 90 kwa Timu ya Matongo Fc kuibuka dhidi ya Mampando Fc.
Waziri Bashungwa ameonyesha kufurahishwa na Taarifa ya Mashindano hayo na kumpongeza mdhamini wa ligi hiyo Mhe. Miraji Mtaturu kwa jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo Jimboni humo.
"Kipekee niseme tu niwe mshuhuda hata Bungeni Mhe. Mtaturu amekua akijenga hoja zenye masilahi kwa wananchi wake na hata akiomba Mradi unaohusu Jimbo Basi ukiwa Waziri wa Wizara aliyoomba Jambo utamuona akifuatilia Hatua zote ili Kuhakikisha alichokiomba kinawafikia Wananchi wake" Alisema Mhe. Bashungwa
Aidha, Mhe. Bashungwa Amesema anamshukuru Mbunge huyo kwa niaba ya wizara kwa kuunga mkono shughuli za michezo ikiwemo kugawa jezi na vifaa vingine ili kuinua michezo kwa vijana, Ambapo amewataka Wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki kuendelea kumuunga mkono Mbunge wao na Mhe. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi kubwa anazozifanya Katika kuliletea Jimbo hilo Maendeleo na Taifa kwa Ujumla.
Pamoja na Mambo mengine Waziri Bashungwa Amekabidhi Zawadi kwa Washindi wa Ligi hiyo ambapo
Mshindi wa kwanza amepata
Kombe, Jezi Set 1, Mpira 1 na taslim sh 1,500,000/=
Mshindi wa Pili Mpira 1 na sh 700,000/= Mshindi wa tatu Mpira 1 na Sh 400,000/= Mshindi wa nne
Sh 150,000/= na Mshindi wa tano
Sh 100,000/=
Aidha, Mfungaji bora Amepata Viatu na sh 100,000/= Mchezaji Bora Sh 100,000/= na Golikipa bora
Gloves na sh 100,000/=
Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni Rasmi kuzungumza mbele ya mamia ya wananchi waliofurika uwanjani hapo Mhe Miraji Mtaturu Mbunge Jimbo la Singida Mashariki alimjulisha Mhe. Waziri kuwa ligi hiyo alianzisha kwa lengo la kuwaunganisha vijana na kuibua vipaji Ambapo Ligi ilishirikisha timu 20 toka kwenye kata zote 13 za jimbo hilo na Kumshukuru kwa kuwa Miongoni mwa Mawaziri wasikivu na wanao fikika na kuongeza kuwa Anaishukuru Wizara hiyo kwa kuona Ni Vema Waziri kwenda Kuhitkmisha ligi hiyo.
Wa upande wake Katibu wa kamati ya mashindano Benno msanga akisoma risala alimueleza mgeni rasmi kuwa wamemshukuru Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Mtaturu kwa kudhamini ligi hiyo pamoja na kugawa jezi na mipira kwa vijiji vyote 50 kwenye kata 13. Ambapo Amegharimia uendeshaji wa ligi kuwalipia waamuzi wenye sifa usafiri kwenda maeneo yalipopangiwa ratiba ya mashindano na kufanya Michezo hiyo kuwa salama na kutoleta fujo Kati ya waamuzi na Wachezaji.
Washabiki wa Timu zote mbili wakitizama Mechi ikiendelea.
Kwa umahiri Line 2 akiendelea kumsaidia Refa wa Mchezo huo.
Ulinzi ukiimarishwa katika Uwanja wa Mpira Shule ya Sekondari Ikungi.
Katibu wa Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ikungi Mwl. Mwendwa akifuatilia Mechi kwa umakini mkubwa.
#bazotvnews
#michezotanzania
#bazilmjungu
#bazotvonline
#ikungi
#singidamashariki
#mtaturu
💪💪
ReplyDelete