Posts

Showing posts from November, 2018

SINGIDA: TIA WASHEREHEKEA MAHAFALI YA KUMI NA SITA (16) KAMPASI YA SINGIDA, MWANZA NA KIGOMA.

Image
Chuo cha Uhasibu Mkoa wa Singida (TIA) leo tarehe 30.11.2018 wamefanya Mahafali ya kumi na sita (16) kwa Kampasi za Singida, Mwanza na Kigoma, ikiwa ni baada ya Wanafunzi kuhitimu Kozi mbalimbali chuoni hapo. Mgeni Rasmi Mhe. Mohammed Mtonga. Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, akihutubia katika Mahafali hiyo amewapongeza Wanafunzi waliofanikiwa Kuhitimu masomo yao, kwani wapo ambao walipenda kuhitimu ila hawakufanikiwa Kwa mambo mbalimbali yaliyo wasibu na kuwakosesha hitaji lao, Mgeni Rasmi  Mhe. Mohammed Mtonga.  amewapongeza Walimu na Bodi ya Chuo kwa ushirikiano walio nao na kwa kuweza kukifikisha Chuo hapo kilipo,  Aidha,  Mgeni Rasmi Mhe. Mohammed Mtonga. Ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayo ongozwa na Kipenzi cha wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Mgufuli kwa kuendelea Kutoa huduma mbalimbali kwa wa Tanzania ikiwemo ya kuhudumia Vyuo mbalimbali Nchini. Mhe. Mohammed Mtonga. Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali. Ambaye ndiye Mgeni Rasmi akihutubia umati

IKUNGI: DC MTATURU AMEENDELEA NA ZIARA YAKE YA KAZI KUKAGUA MIRADI NA KUFANYA MIKUTANO YA HADHARA KATA YA SIUYU.

Image
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu amefanya ziara katika Kijiji cha Unyankhanya kilichopo Kata ya Siuyu Wilayani Ikungi ambapo k atika ziara hiyo  DC Mtaturu. ameongea na Wananchi kwenye Mkutano wa hadhara na kukagua Miradi na kuamuru kuhamishwa kwa Dkt.  Donata shayo  Mganga mkuu wa Zahanati ya Unyankhanya, baada ya wananchi kulalamika mbele ya DC Mtaturu kwenye Mkutano wa hadhara. Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, amewataka wananchi wa Kijiji cha Unyankhanya kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Serikali ya Kijiji ili kuweza kumalizia viporo vya Miradi iliyosimama kwa muda mrefu. "Naomba niwaambie Ndugu wananchi wa Unyankhanya na Kata ya Siuyu, kuna watu hawaja tafsiri vizuri neno Elimu Bure,  Elimu bure imelenga kuondoa ada iliyokuwwa kikwazo kwa watoto kupaka haki yao ya kupata Elimu na W azazi kupitia kamati ya shule wanaowajibu kujua mapungufu na kuweka utaratibu wa kuchangia kwa mujibu wa waraka wa Elimu wa Mwaka 2016.a Mzazi, Mlezi au Mwananchi kuchangia maendel

SHINYANGA: NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE. DOTO BITEKO (MB) ATEMBELEA MGODI WA BUZWAGI

Image
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (MB) amefanya ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi uliopo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga lengo likiwa ni kukagua shughuli za uchimbaji Madini, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali  zinazoukabili mgodi huo, Katika ziara hiyo Naibu Waziri Biteko aliambatana na  Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Ndg. Timothy Ndaya,  Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kahama, Mhandisi Abdulrahman Milandu, Afisa Mgodi Mkazi wa Mkoa wa Kahama, Modest Tarimo, Mkaguzi wa Migodi kutoka Tume ya Madini Mhandisi Frederick Mwanjisi, wataalam kutoka Wizara ya Madini. Mara baada ya  kufanya ziara na kupokea taarifa ya hatua za kufunga mgodi wa Buzwagi, Naibu Waziri Biteko alitoa  maagizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na:- Mgodi kuwasilisha upya mpango wa ufungaji wa shughuli zake kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini ili aweze kuwasilisha kwenye Kamati ya Kitaifa ya U

IKUNGI: DC MTATURU AMFUTIA MKATABA MASHANJALA AMBAYE NI MKANDARASI WA JENGO LA ZAHANATI MNYANGE KWA KULITELEKEZA KWA MIAKA 7.

Image
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu Ameagiza kusimamishwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Kijiji cha Mnyange na Mkandarasi Aliyejulikana kwa jina moja la MASHANJALA aliyekua akijenga Zahanati ya Kijiji aliyesababisha ujenzi kusimama kwa muda wa miaka saba (7). Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jirani na eneo la jengo hilo la Zahanati, DC Mtaturu amewataka Serikali ya Kijiji kuwa karibu na wananchi ili kushirikishana kutatua changamoto za maendeleo kwa pamoja, kwani kutowashirikisha wananchi ndiyo chanzo cha kupoteza uaminifu kwa viongozi wao. Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu Amewataka Wananchi wa Kijiji cha Mnyange kuendelea kuwa na subira kwani Serikali inayo ongozwa na Rais wa Wanyonge Dkt John Pombe Magufuli aliahidi kuwatumikia wananchi wote kwa usawa bila ubaguzi na kuhakikisha zinajengwa Zahanati kila Kijiji Tanzania ili kuhakikisha kunatokomezwa kwa tatizo la kufariki kwa Mama na Mtoto na kutoa huduma kwa Wazee. N