IKUNGI: DC MTATURU AMEONGOZA HARAMBEE YA UPATIKANAJI WA PIKIPIKI KWA AJILI YA WACHUNGAJI NA KUPATIKANA PIKIPIKI 5 NA TSH 2.557,300.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu ameongoza harambee ya kupata Pikipiki kwa aijili ya usafiri wa Wachungaji katika Kanisa la Fpct Makiungu.Harambee iliyowepelekea kupatikana kwa Pikipiki tano (5) ta fedha tsh 2,557,300/=.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ikungi Ndg. Justice Lawrence Kijazi akikabidhi mchango wake WA Pikipiki moja (1).
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ikungi Ndg. Justice Lawrence Kijazi akiwashukuru wananchi kwa kutaimbua Serikali na kuishirikisha katika shughuli za Kanisa. "Ninawapongeza na kuwashukuru viongozi WA kanisa, kwa kutambua umuhimu wa Serikali na kuishirikisha katika shughuli zenu na ninawaahidi Ofisi ya Mkurugenzi itawapa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha changamoto zinazo wakabili zinapungua".
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Ndg Solomon Kasaba akikabidhi mchango wa Chama wa Pikipiki moja (1) Ikiwa na mchango wa Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha Wachungaji wanawafikia waumini wao kwa wakati.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Ndg Solomon Kasaba akiwashukuru kwa dhati Wachungaji na waumini kwa kutambua uwepo wa Chama Cha Mapinduzi na Kuendelea kukiamini siku hadi Siku na kamwe Chama Cha Mapinduzi hakitawaangusha katika mahitaji yenu ya Kanisa.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu Akimkabidhi Askofu wa Fpct Jimbo la Singida fedha zilizopatika kwa kwenye harambee.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu Akimshukuru Askofu kwa mchango wao wa maombi ya kuiombea Serikali na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu akiwashukuru waumini na Wachungaji kwa kujitoa kwa Mungu na kuweza kumtolea sadaka na kuweza kupatikana kwa Pikipiki na fedha.
Aidha DC Mtaturu amewahimiza waumini na wasio waumini kuwa Serikali itaendelea kuwaletea huduma stahiki kama Maji na Umeme na Huduma za Elimu bila malipo ikiendelea kutolewa na Serikali bila ubaguzi wowote.
Mwisho.
Comments
Post a Comment