IKUNGI: DC MTATURU AMEENDELEA NA ZIARA YAKE YA KAZI KUKAGUA MIRADI NA KUFANYA MIKUTANO YA HADHARA KATA YA SIUYU.


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu amefanya ziara katika Kijiji cha Unyankhanya kilichopo Kata ya Siuyu Wilayani Ikungi ambapo katika ziara hiyo  DC Mtaturu. ameongea na Wananchi kwenye Mkutano wa hadhara na kukagua Miradi na kuamuru kuhamishwa kwa Dkt. Donata shayo Mganga mkuu wa Zahanati ya Unyankhanya, baada ya wananchi kulalamika mbele ya DC Mtaturu kwenye Mkutano wa hadhara.

Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, amewataka wananchi wa Kijiji cha Unyankhanya kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Serikali ya Kijiji ili kuweza kumalizia viporo vya Miradi iliyosimama kwa muda mrefu.

"Naomba niwaambie Ndugu wananchi wa Unyankhanya na Kata ya Siuyu, kuna watu hawaja tafsiri vizuri neno Elimu Bure,  Elimu bure imelenga kuondoa ada iliyokuwwa kikwazo kwa watoto kupaka haki yao ya kupata Elimu na Wazazi kupitia kamati ya shule wanaowajibu kujua mapungufu na kuweka utaratibu wa kuchangia kwa mujibu wa waraka wa Elimu wa Mwaka 2016.a Mzazi, Mlezi au Mwananchi kuchangia maendeleo ya Kijiji chake, kwahiyo niwaase kwamba tuwahasaidie watoto wetu kupata mazingira bora ya kusomea na kwa hakika na sisi Serikali ya Wilaya tutaweka mkono wetu, hivyo ninatoa mifuko ishirini ya Saruji na Matofali Elfu moja kwa ajili ya ujenzi wa Matundu ya vyoo na hadi January 2019 viwe vimekamilika.

Dc Mtaturu, Akiongea kwa msisitizo amesema neno Elimu bure imelenga kuondoa ada iliyokuwwa kikwazo kwa watoto kupaka haki yao ya kupata Elimu na wazazi kupitia kamati ya shule wanaowajibu kujua mapungufu na kuweka utaratibu wa kuchangia kwa mujibu wa waraka wa Elimu wa Mwaka 2016.

Wananchi wakisikiliza kwa makini hutuba ya Mhe. DC Mtaturu.

Wananchi wakisikiliza hutuba ya Mhe. DC Mtaturu.

DC Mtaturu, Katika Mkutano wa Kijiji cha Unyankhanya amewachangia Mifuko Ishirini ya Saruji (20) na Matofali ya Block elfu moja (1000) Ili kuwaongezea nguvu wananchi ikiwa ni kuwasukuma katika Kumalizia ujenzi wa Vyoo vya Wanafunzi.

DC Mtaturu, akikagua Sehemu ya kunawia Wanafunzi wanapokua wametoka chooni.

DC Mtaturu akikagua shimo la Choo cha wanafunzi cha shule ya Msingi Unyankhanya ambacho ameagiza kumalizika Mara moja.

DC Mtaturu, Hakuishia hapo alienda hadi Shule ya Sekondari Siuyu na kwenda kukagua ujenzi wa Maabara na Madarasa mapya.

DC Mtaturu, akaenda kufanya Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Siuyu.

DC Mtaturu, Akihutubia wananchi wa Kijiji cha Siuyu Madukani.

DC Mtaturu, ametoa agizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, kumuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya Kutoa Nesi Mmoja kwa ajili ya Huduma ya Mama na Mtoto atakaye hudumia kwenye jengo la muda ambalo ameteua jengo la Vijana Siuyu.

Aidha DC Mtaturu, amewahimiza Wazazi/Walezi kutoa huduma ya Lishe Shuleni ili kumfanya mwanafunzi kuwa na uelewa wa haraka tofauti na kuwashindisha njaa Watoto na kuwafanya wasifanye vizuri katika masomo.

MWISHO.

@bazilmjungu#



Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida