KAMPUNI YA BIOSUSTAIN WAMEENDELEA KUTOA MAFUNZO YA KILIMO BORA CHA PAMBA WILAYANI IKUNGI

BIOSUSTAIN ni Kampuni inayojishugulisha na ununuaji na uchambuaji Pamba Yenye makao makuu yake MKOANI Singida, Imeanza kutoa mafunzo Vijiiini Kuhusu Kilimo bora cha Pamba na kuwakumbusha wakulima kuzingatia msimu vizuri.

Ndg. Matutu Afisa Kilimo wa Kampuni ya Biosustain akielekeza wakulima jinsi ya kutega wadudu waharibifu shambani na kuifanya Pamba kwa na afya ili kutoa bidhaa iliyo bora.

Ndg. Azizi Abeid Meneja Mradi akiwahakikishia wakulima kuhusu soko la PAMBA kua ni la uhakika na halina dalali. "Kwanza niwakumbushe na kuwaambia ukweli kuhusu Pamba, Pamba Ukizingatia upandaji na kuzuia wadudu lazima uondokane na umaskini, Pamba ni zao lenye uhakika mkubwa na maradufu kwa mkulima"

Aidha Ndg. Azizi Abeid ambaye ni Meneja Mradi amewasisitiza wananchi kulima pamba kwa wingi ili kuweza kujikimu kimaisha.

Ndg. Azizi Abeid Meneja Mradi.

Wananchi wakisikiliza kwa umakini mkubwa mafunzo ya Kilimo bora cha Pamba.

Mwananchi akiishukuru kampuni ya Biosustain kwa kuwapa elimu ya Pamba kwani wamekua wakilima Pamba bila utaratibu na kujikuta wakipata faida kidogo, Aidha Mwananchi huyo amewashukuru Biosustain kwa kuwa wanawapatia Mbegu na Dawa ya kuua wadudu.

MWISHO.


Comments

  1. Jina la huyo Mkulima ni nani na anatoka kijiji kipi. Hilo ni muhimu pia unapotoa taarifa kama hiyoo. Maana ameongea jambo Jema.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida