SINGIDA: MKUU WA MKOA WA SINGIDA DKT. REHEMA NCHIMBI AZINDUA KAMPENI YA “JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA”
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi. Akisisitiza taarifa inavyoonyesha hali halisi ilivyo sasa katika masuala yanayohusu uzazi salama wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” iliyofanyika Ukumbi wa Singida DC.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi. Akisaini mkataba maalum ambao ametiliana saini na Wakuu wa Wilaya zote za Singida ikiwa ni kuhakikisha mkataba huo unazingatiwa na kufanya utekelezaji uliotukuka.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi. Amewasisitiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Waganga Wakuu wahakikishe wanayafanya aliyoyaagiza na ikiwa ni kutekeleza Agizo la Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu. Aliyeanzisha kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama”
"Na niseme tu kwa upendo wa dhati kuonyesha tunawajali kina Mama na Watoto ni lazima tuwe na mkakati wa KUSHUKA JUMLA JUMLA na watumishi ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo na badala yake kusababisha vifo vya Mama na Mtoto, Sitakubali na ninasema sitakubali Wakuu wa Wilaya Tushuke Jumla Jumla kwa hao wazembe wahache wanao haribu sifa za Serikali yetu inayo ongozwa na Kipenzi cha watu Dkt. John Pombe Magufuli tusikubali kabisa, kwahivo naagiza mkafanye na ionekane mnafanya na mmefanya.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi. akimkabidhi vitendea kazi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu (Kushoto) mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama”
Sehemu ya Wageni kutoka Taasisi za Dini waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Singida DC.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Justice Lawrence (katikati) akisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Singida DC.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi. akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri baada ya kumaliza Uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama”
MWISHO.
@bazilmjungu#
Comments
Post a Comment