Posts

Showing posts from February, 2023

HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI YATOA MIKOPO YA 10% SHILINGI MILIONI 141 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE VIJANA NA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM

Image
Na Bazil Mjungu Singida: Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida imetoa mikopo ya asilimia kumi (10%) kutoka kwenye mapato yake ya ndani ya Shilingi milioni miamoja arobaini na Moja (141) na Verehani tatu katika Vikundi kumi na mbili vya Wanawake, Vijana na watu wenye mahitaji Maalum. Vikundi vilivyo nufaika ni Pamoja  na vya Wanawake ambavyo ni kikundi Cha Ushirika Cha Siuyu, Kikundi cha Jonelaa cha Siuyu, Kikundi cha Heshima Wanawake cha Ikungi, Tumaini Stara Cha Iyumbu, Kikundi cha Mshikamano cha Iyumbu, Kikundi cha Faraja cha Mgungira, Kikundi cha Igembensabo cha Ng'ongosoro, Kikundi cha Ipililo cha Ng'ongosoro sambamba na Vikundi vya Vijana ambavyo ni Kikundi cha Kidundu cha Kipunda, Kikundi cha Roho safi cha Iyumbu, Kikundi cha Be the Light cha Kipumbuiko, Kikundi cha Vijana Chapakazi cha Ikungi na Kikundi Cha Walemavu cha Kwajaa cha Matongo, Aidha, Mikopo hii imetolewa Leo February 7 kutoka kwenye nusu ya kwanza ya Bajeti ya Mwaka 2022/2023 Kama mchango wa asili