Posts

Showing posts from January, 2020

UWT UKEREWE KUSAKA KURA ZA RAIS DKT MAGUFULI, MBUNGE NA MADIWANI KUPATA USHINDI WA KISHINDO

Image
Na Peter Fabian Ukerewe. Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wa Wilaya ya Ukerewe wameahidi kumuunga mkona Mwenyekiti wa CCM taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kushinda kwa kishindo uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu 2020. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa UWT Wilaya hiyo Spelancia Nagabona wakati wa hafla ya kupokea Baiskeli 59 za wenyeviti na makatibu wa Jumuiya hiyo wa Kata 25 za Jimbo la Wilaya ya Ukerewe zilizotolewa na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Mwanza Kemilembe Lwota na kukabidhiwa mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la UWT Wilaya. Mwenyekiti Nagabona aliwaeleza wajumbe wa Baraza hilo kuwa baiskeli hizo zitakabidhiwa kwa kila Mwenyekiti na katibu wa Jumuiya hiyo wa Kata zote 25 ili kuwasaidia usafiri wa kuwafikia wanachama wa ngazi za matawi na kuhamasisha wananchi ili kuwachagua wagombea watakaopitishwa na CCM kugombea Ubunge na Udiwani huku wakihakikisha wanampigia debe Rais Dkt Magufuli achaguliwe t