Posts

Showing posts from June, 2019

DC MTATURU KUGHARAMIA MASOMO YA MWANAFUNZI FAIDHA NTANDU KIDATO CHATANO NA SITA

Image
MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mh Miraji Mtaturu ameamua kugharamia masomo ya mwanafunzi Faidha Ntandu ya kidato cha tano na sita. Mwanafunzi huyo amemaliza kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Unyahati na kufaulu kwa daraja la kwanza katika masomo ya sayansi. Faidha kwa sasa analelewa na mama yake mkubwa Sitta Dude baada ya mama yake mzazi kufariki dunia. Kutokana na ufaulu huo amepangiwa kujiunga kidato cha Tano shule ya Sekondari Karema wilayani Mpanda mkoani Katavi kwa mwaka wa masomo 2019/2020. Akizungumza ofisini kwake na mwanafunzi huyo aliyeambatana na mama yake mkubwa, mh Mtaturu amesema ameguswa na juhudi za mtoto huyo.  “Nakupongeza mtoto wangu kwa kufanya vizuri katika masomo yako,najua changamoto unazozipitia,kama kiongozi wa serikali katika wilaya hii niahidi kuwa  nitagharamia masomo yako mpaka utakapomaliza kidato cha sita,”alisema mh Mtaturu. Amesema serikali inaweka mikakati mbalimbali ya kumlinda mtoto wa kike ili atimize