Posts

Showing posts from December, 2022

MASHINDANO YA MPIRA WA WAVU YA MAVUNDE CUP YAZINDULIWA RASMI LEO JIJINI DODOMA

Image
Na Mwandishi wetu Dodoma: Mashindano ya mpira wa wavu maarufu kama * MAVUNDE CUP * yamezinduliwa rasmi leo katika shule ya Msingi Mlezi Jijini Dodoma huku yakijumuisha Timu 18 za wanaume na wanawake kutoka mkoani Dodoma na nje ya Dodoma. Mashindano hayo yamezinduliwa leo na Diwani wa Kata ya Hazina * Mh. Samwel Mziba * akiongozana na Diwani wa Viti Maalum * Mh. Flora Lyacho * huku wote wakitoa rai kwa Vijana wa Dodoma kuchukua fursa ya haya mashindano kama sehemu ya kuendeleza na kukuza vipaji vyao. Aidha zoezi hili la uzinduzi wa mashindano limekwenda sambamba na ugawaji wa vifaa vya michezo kwa Timu zote zinazoshiriki katika mashindano hayo pamoja na ukarabati wa kiwanja cha kuchezea. Mashindano hayo yatafikia tamati tarehe * 01.01.2023 * siku ya Jumapili, ambapo Mgeni Rasmi wa mashindano hayo anatarajiwa kuwa * Mh. Anthony Mavunde * Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Mfadhili wa mashindano hayo. #bazotvnews.

DARASA NA STREETLECTURE UTAJIRI na UMASIKINI

Image
Na Shaabani Y. Shaabani : Utajiri haimaanishi kuwa na akaunti ya benki nono. Utajiri kimsingi ni uwezo wa kutengeneza mali. Mfano: Mtu anayeshinda bahati nasibu au kamari. Hata akishinda milioni 100 si tajiri: Ni maskini mwenye pesa nyingi. Ndiyo sababu 90% ya mamilionea wa bahati nasibu wanakuwa maskini tena baada ya miaka 5. Pia una matajiri ambao hawana pesa. Mfano:Wajasiriamali wengi. TAYARI wapo njiani kuelekea kwenye utajiri japokuwa hawana pesa, maana wanakuza akili zao za fedha na huo ndio utajiri. * Tajiri na maskini wanatofauti gani? * Kwa maneno rahisi: Tajiri anaweza kufa ili kuwa tajiri na hutumia mda wake mwingi kujigunza na na ya kupiga hatua zaidi, Na maskini anaweza kuua ili kuwa tajiri na hutumia mda wake mwingi kusengenya,kueneza chuki,Ubinafsi na Kuwaza Uwasherati. Ukiona kijana anaamua kufundisha, kujifunza mambo mapya, ambaye anajaribu kujiboresha mara kwa mara, ujue kwamba yeye ni tajiri. Ukiona kijana anafikiri kuwa tatizo ni serikali, na anayedhani ku