Posts

Showing posts from November, 2022

MTATURU ATAHADHARISHA KANUNI ZA SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI.

Image
Na Bazil Mjungu Dodoma: MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki (CCM), Mhe. Miraji Mtaturu, ametahadharisha kanuni zitakazotungwa kwenye muswada wa sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi wa mwaka 2022  kuhakikisha zinaendana na sheria ili zisiibue malalamiko kwa wananchi. Akichangia leo bungeni, Mtaturu amesema sheria hiyo ni nzuri lakini utungaji wa kanuni hizo uendane na sheria iliyopitishwa. “ Pamoja na sheria hii kuwa nzuri na tumekuwa tukipitisha hapa, kumekuwa na changamoto ya kanuni, niombe sana kwenye eneo hili na sisi tunamuamini Waziri, sheria ikitungwa nzuri iende hivyo hivyo na kanuni ziwe nzuri,” amesema Mtaturu. Mtaturu amesema eneo la utungaji wa kanuni linaweza kuwa mwiba mwingine katika utekelezaji wa sheria zinazopitishwa na bunge. “ Tumekuwa tukipitisha baadhi ya sheria lakini ile nafasi ya kutengeneza kanuni huwa inakwenda kuharibu kabisa sheria, matokeo yake wabunge tunaulizwa mlipitishaji sheria hii, kumbe kanuni imekwenda kuharibu kabisa maudhui mazima ya sheria ambayo