Posts

Showing posts from October, 2021

MAVUNDE AKABIDHI TV NA KING'AMUZI SHULE YA SEKONDARI MPUNGUZI

Image
Na Bazil Mjungu Dodoma: Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde leo Tarehe 29 October 2021 Amezungumza na wanafaunzi wa Shule ya Sekondari Mpunguzi na kuwapatia mrejesho wa Huduma zinazo letwa na Serikali  ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Mara baada ya Mazungumzo mazuri na Wanafunzi hao Mbunge huyo amewakabidhi Televisheni na King’amuzi cha Azam vyote vyeye Thamani ya Shilingi 1,745,000 kwa lengo la kuwapa Nafasi ya kujifunza zaidi na kupata habari mbalimbali za Nchi na za Kimataifa Pamoja  na kufuatilia kwa karibu Utendaji kazi wa Viongozi wa Serikali walio wachagua. Aidha, Mhe. Mavunde ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa madarasa 6 shuleni hapo yenye thamani ya Shilingi 120,000,000 na yeye kuahidi kuzisimamia kwa karibu na kikamilifu ili zilete matokeo yaliyokusudiwa. #antonymavunde #ssh #ikulutanzania #bazotvnews #bazotvonline #kaziiendelee #a

UFUNGUZI KIKAO CHA UWEKEZAJI WILAYA YA IKUNGI KILIMO CHA ALIZETI CHAPEWA KIPAUMBELE

Image
Na Bazil Mjungu Singida: Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Jerry Muro leo Tarehe 29 October 2021 amefungua kikao Cha Uwekezaji Katika sekita ya Kilimo Wilaya ya Ikungi. Katika kikao hicho Kaimu Mkuu wa Mkoa amesema uwekezaji katika kilimo wao wameona Ni vema kuanza na Uwekezaji wa Kilimo cha zao la Alizeti. Pamoja na Mambo mengine Kaimu Mkuu wa mkoa wa Singida Jerry Murro amesema halmashauri ya Wilaya ya Ikungi imetenga ekari zaidi ya laki Moja kwa ajili ya kilimo cha alizeti. Aidha Mhe Jerry Muro amesema tayari Wizara ya kilimo imeshatoa Mbegu bora za kilimo kiasi cha tani elfu 13 kwa ajili ya wakulima wa alizeti Wilayani Ikungi. Wajumbe wa  Kikao cha Uwekezaji Wakisikiliza Hotuba ya kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Jerry Muro. Ras Mstaafu Alhaji Salum Chima kushoto na Mkurugenzi wa JMC Eng. Msafiri wakisikiliza Hotuba ya Ufunguzi wa Kikao cha Uwekezaji. Wadau wa Kilimo wakisikiliza Hotuba ya Ufunguzi wa Kikao cha Uwekezaji iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Jerry Muro.

MHE. ANTONY MAVUNDE KUFANIKISHA UJENZI WA UZIO SHULE YA SEKONDARI DODOMA

Image
Na Bazil Mjungu Dodoma: Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini   Mhe. Anthony Mavunde ameahidi kufanikisha Ujenzi wa Uzio wa Shule ya Sekondari Dodoma kwa lengo la kuongeza Ulinzi kwa wanafunzi na mali za shule hiyo. Mbunge Mavunde ameyasema hayo leo Tarehe 29 October 2021 wakati wa hafla ya Mahafali ya kidato cha IV shuleni hapo kufuatia maombi yaliyowasilishwa na wanafunzi kupitia Risala iliyosomwa mbele yake. Mhe Mavunde amesema Atahakikisha analifanyia kazi swala hilo ikiwa ni yeye Mbunge na kwa kushirikiana na Wadau wa Elimu Lazima Miundombinu ya Shule zote Katika Jimbo la Dodoma Mjini zinakua zinaridhisha wakati wote. “ Nataka niwahakikishie Wanafunzi, Walimu na Wazazi kwamba tutamalizia ujenzi wa eneo la uzio lililobaki ili kulizungushia eneo lote la shule na uzio kwa madhumuni ya usalama wa wanafunzi na mali zote zilizopo shuleni tunashukuru kazi kubwa iliyofanywa na wanafunzi waliosoma hapa wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndg. Masanja Kadogosa kwa ujenzi wa uzio kwa awamu ya kw

SERIKALI YATENGA SH. BILIONI 170 UJENZI MKONGO WA TAIFA

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imetenga shilingi bilioni 170 kwa ajili ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa katika mwaka wa fedha 2021/2022. “Lengo letu ni kuwawezesha watoa huduma za mawasiliano kutumia miundombinu hii kuboresha huduma za mawasiliano nchini na kurahisisha ufikishwaji wa intaneti kwenye ofisi mbalimbali za sekta ya umma na binafsi” Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Oktoba 22, 2021) wakati alipofungua Mkutano wa Tano wa Mwaka wa TEHAMA Tanzania uliofanyika katika katika ukumbi wa mikutano wa AICC, jijini Arusha. Amesema fedha hizo zitawezesha kujenga kilomita 4,244 za Mkongo ili kufikisha jumla ya kilomita 12,563. Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuiagiza Wizara ya Habari, Sayansi na Teknolojia ya Habari isimamie kwa karibu mradi wa upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili wananchi wengi zaidi washiriki katika ujenzi wa uchumi wa kidijitali. “Hivi

RC SINGIDA: DKT MAHENGE APONGEZA IKUNGI TEAM WORK

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge leo Oct 19/2021 amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Ikungi Mkoani humo ambapo ametembelea Miradi ya Mbalimbali ya Maendeleo  ikiwemo Skimu ya Umwagiliaji Katika Kijiji cha Mang'onyi na kukagua Ujenzi wa Madarasa katika Shule ya Sekondari ya Mwau Sambamba na kuzindua rasmi  Msimu wa Kilimo katika Mkoa wa Singida wakati alipokua akihutubia Wananchi wa kata ya Issuna. Mheshimiwa Mahenge ameupongeza Ushirikiano uliopo baina ya Viongozi wa Wilaya ya Ikungi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Jerry Muro, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndugu Justice Lawrence Kijazi wakuu wa Idara na kusema Umoja huo Unapaswa kuigwa na kusisitiza kuwa mshikamano huo Unapaswa  kuendelezwa kwa maslahi ya mapana ya Maendeleo ya Wananchi wa Wilaya ya Ikungi na Taifa kwa Ujumla. Mheshimiwa Mahenge amewataka Wananchi wa Wilaya ya Ikungi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa