MAVUNDE AKABIDHI TV NA KING'AMUZI SHULE YA SEKONDARI MPUNGUZI

Na Bazil Mjungu Dodoma:

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde leo Tarehe 29 October 2021 Amezungumza na wanafaunzi wa Shule ya Sekondari Mpunguzi na kuwapatia mrejesho wa Huduma zinazo letwa na Serikali  ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.


Mara baada ya Mazungumzo mazuri na Wanafunzi hao Mbunge huyo amewakabidhi Televisheni na King’amuzi cha Azam vyote vyeye Thamani ya Shilingi 1,745,000 kwa lengo la kuwapa Nafasi ya kujifunza zaidi na kupata habari mbalimbali za Nchi na za Kimataifa Pamoja  na kufuatilia kwa karibu Utendaji kazi wa Viongozi wa Serikali walio wachagua.


Aidha, Mhe. Mavunde ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa madarasa 6 shuleni hapo yenye thamani ya Shilingi 120,000,000 na yeye kuahidi kuzisimamia kwa karibu na kikamilifu ili zilete matokeo yaliyokusudiwa.

#antonymavunde
#ssh
#ikulutanzania
#bazotvnews
#bazotvonline
#kaziiendelee
#azanews
#tbc
#itv
#dodoma
#jimbododomamjini


Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida