MHE. ANTONY MAVUNDE KUFANIKISHA UJENZI WA UZIO SHULE YA SEKONDARI DODOMA

Na Bazil Mjungu Dodoma:
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini   Mhe. Anthony Mavunde ameahidi kufanikisha Ujenzi wa Uzio wa Shule ya Sekondari Dodoma kwa lengo la kuongeza Ulinzi kwa wanafunzi na mali za shule hiyo.

Mbunge Mavunde ameyasema hayo leo Tarehe 29 October 2021 wakati wa hafla ya Mahafali ya kidato cha IV shuleni hapo kufuatia maombi yaliyowasilishwa na wanafunzi kupitia Risala iliyosomwa mbele yake.

Mhe Mavunde amesema Atahakikisha analifanyia kazi swala hilo ikiwa ni yeye Mbunge na kwa kushirikiana na Wadau wa Elimu Lazima Miundombinu ya Shule zote Katika Jimbo la Dodoma Mjini zinakua zinaridhisha wakati wote.


Nataka niwahakikishie Wanafunzi, Walimu na Wazazi kwamba tutamalizia ujenzi wa eneo la uzio lililobaki ili kulizungushia eneo lote la shule na uzio kwa madhumuni ya usalama wa wanafunzi na mali zote zilizopo shuleni tunashukuru kazi kubwa iliyofanywa na wanafunzi waliosoma hapa wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndg. Masanja Kadogosa kwa ujenzi wa uzio kwa awamu ya kwanza nawahakikishia kwamba tutamalizia palipobaki: Amesema Antony Mavunde

Kwa upande mwingine Mhe. Mavunde ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Shule hiyi kiasi cha Shilingi Milioni 60 kwaajili ya ujenzi wa Madarasa Matatu ambayo yatasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa Katika Shule hiyo.

Akitoa maelezo ya awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Dodoma, Aman Mfaume ameelezea mikakati ya kitaaluma ambayo shule imejiwekea ikiwa ni pamoja na kuwa na masomo ya ziada (Remedial Classes) ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wananafanya vizuri katika mitihani yao ya Taifa na hivyo kuijengea sifa Wilaya ya Dodoma Mjini na Mkoa kwa ujumla.


Wanafunzi Wakimsikiliza Hotuba ya Mgeni Rasmi Katika Hafla hiyo, Mhe. Antony Mavunde.


Mhe. Mavunde akikabidhi Mipira kwa Wanafunzi  kwa ajili ya kuimarisha Michezi Shuleni.

#bazotvonews




Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida