Posts

Showing posts from November, 2019

MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA GEITA MHE. VICKY KAMATA AMEUNGA MKONO JUHUDI ZINAZOFANYWA NA RAIS MAGUFULI ZA TANZANIA YA VIWANDA KWA KUKABIDHI VITU VYENYE THAMANI YA MILIONI 125. MKOANI GEITA.

Image
Na. Bazil Mjungu: Geita. Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Geita Mhe.Vicky Kamata ameunga mkono  juhudi zinazofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwa Tanzania ya Viwanda kwa kutoa Vyerehani 350 kwa Kata zote za Mkoa  wa Geita. Vyerehani hivyo vyenye Thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 87.5 vimetolewa kwa Kata zote za Mkoa wa Geita.  Pamoja na Vyerehani hivyo, Mbunge Vicky Kamata amekabidhi Shilingi Milioni 17.5 kwa  ajili ya kutunisha Saccos za Akina Mama wa kata zote za mkoa wa Geita. Sambamba na hilo Mh. Vicky Kamata ametoa Chupa za Chai  360 kwa akina mama kwa ajili ya kuinua mitaji ya baadhi ya wamama lishe ili kusaidia kuinua vipato vyao. Akikabidhi vyerehani, fedha pamoja na chupa za chai kwa akina Mama hao Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabrieli amempongeza Mh. Vicky Kamata (Mb) kwa upendo aliounyesha kwa kina mama na kwa jamii ya wananchi wa Mkoa wa Geita kwa kuwajali wanawake na kuwapa ushirikiano mkubwa katika kuleta maendeleo. &q

SINGIDA: MBUNGE SIMA AKABIDHI MASHINE YA PHOTOKOPI YA ZAIDI YA MILIONI 3, NA MIFUKO 300 YA SARUJI KUSAIDIA UJENZI KITUO CHA AFYA KISAKI

Image
Na Shams Kunge. Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Musa Sima amekabidhi Mashine ya kutolea Kopi (Photocopy Machine) yenye thamani ya Milioni tatu (3000,000/= ili kuwapunguzia Wazazi na Walimu garama za kwenda kutoa kopi za kulipia, mashine hiyo ameikabidhi kwenye sherehe ya Mahafali ya Kidato cha Nne 2019 Shule ya Sekondari Mufumbu iliyofanyika Tarehe 17.November 2019. Sambamba na hilo Mhe. Sima amekabidhi Mifuko 300 ya Saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kisaki. "Niwaombe wadogo zangu, wanangu na hususani wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mufumbu vidato vyote someni kwa bidii na msome kwelikweli kwani Elimu kwasasa haina Mbadala na tusitanie kwenye hili, lakini pia niwatake Walimu kuhakikisha mnawalea kikamilifu wanafunzi wetu na hilo sio ombi kwani ninyi ni mashahidi Serikali inatoa fedha nyingi za Elimu bila Malipo na kila mwezi shule inapokea fedha za fidia ya ada na Mahitaji mengine mengi,

SINGIDA: BARAZA LA MADIWANI IKUNGI LAZITAKA KAMPUNI ZILIZONUNUA PAMBA KWA WANANCHI KUWALIPA FEDHA ZAO KABLA YA NOVEMBA 30/2019

Image
SINGIDA:  Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi limezitaka Kampuni zilizonunua Pamba kwa wakulima wilayani humo kuwalipa mara moja wakulima fedha wanazo dai kabla ya mwisho wa mwezi novemba 2019 kwani msimu wa kilimo umefika watashindwa kuandaa mashamba yao kama watakua hawajalipwa fedha hizo. Akiongea kwenye Baraza lililofanyika tarehe 13.11.2019 Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Diwani wa Kata ya Mtunduru Mhe. Ramadhani Mpaki ameitaka Kampuni ya ununuzi Pamba ya Biosustain kufanya hivo mapema ili kutowakatisha tamaa wakulima kuendelea na kilimo hicho, kwa upande wake Makamu Mwenyeketi wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Issuna Mhe. Missai amewataka wakulima kuandaa mashamba yao mapema ili kuwahi msimu wa mvua unatotarajiwa kuanza hivi karibuni. Nae Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Justice Lawrence Kijazi amewahakikishia wakulima kulipwa fedha zao kwani atafuatilia kwa ukaribu maagizo ya Baraza. Swala la kulipwa fedha wakulima Lilijiri baada