MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA GEITA MHE. VICKY KAMATA AMEUNGA MKONO JUHUDI ZINAZOFANYWA NA RAIS MAGUFULI ZA TANZANIA YA VIWANDA KWA KUKABIDHI VITU VYENYE THAMANI YA MILIONI 125. MKOANI GEITA.

Na. Bazil Mjungu: Geita.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Geita Mhe.Vicky Kamata ameunga mkono  juhudi zinazofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwa Tanzania ya Viwanda kwa kutoa Vyerehani 350 kwa Kata zote za Mkoa  wa Geita.

Vyerehani hivyo vyenye Thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 87.5 vimetolewa kwa Kata zote za Mkoa wa Geita. 

Pamoja na Vyerehani hivyo, Mbunge Vicky Kamata amekabidhi Shilingi Milioni 17.5 kwa  ajili ya kutunisha Saccos za Akina Mama wa kata zote za mkoa wa Geita.

Sambamba na hilo Mh. Vicky Kamata ametoa Chupa za Chai  360 kwa akina mama kwa ajili ya kuinua mitaji ya baadhi ya wamama lishe ili kusaidia kuinua vipato vyao.

Akikabidhi vyerehani, fedha pamoja na chupa za chai kwa akina Mama hao Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabrieli amempongeza Mh. Vicky Kamata (Mb) kwa upendo aliounyesha kwa kina mama na kwa jamii ya wananchi wa Mkoa wa Geita kwa kuwajali wanawake na kuwapa ushirikiano mkubwa katika kuleta maendeleo.

"Nakupongeza sana Mh. Vicky Kamata Likwelile kwa kuunga mkono kwa dhati juhudi kubwa za Mh. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli kuifikia Tanzania ya Viwanda na uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, naomba kuwasihi wanawake wa Mkoa wa Geita Mshikamane pamoja na kutumia vizuri fursa hii na fursa  mbalimbali zilizopo katika Mkoa wa Geita." Alisema Injinia Robert Gabrieli. RC GEITA.

Sambamba na jitihada hizo za Tanzania ya Viwanda Mh. Vicky kamata Likwelile akizungumza na akina mama wa Wilaya za Chato, Mbogwe, Bukombe na Geita katika ziara yake ya siku 3 amewasisitizia  umuhimu wa wanawake kuungana na kua kitu kimoja kwa ajili ya Maendeleo yao. 

 #bazotvnews

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida