SINGIDA: MBUNGE SIMA AKABIDHI MASHINE YA PHOTOKOPI YA ZAIDI YA MILIONI 3, NA MIFUKO 300 YA SARUJI KUSAIDIA UJENZI KITUO CHA AFYA KISAKI

Na Shams Kunge.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Musa Sima amekabidhi Mashine ya kutolea Kopi (Photocopy Machine) yenye thamani ya Milioni tatu (3000,000/= ili kuwapunguzia Wazazi na Walimu garama za kwenda kutoa kopi za kulipia, mashine hiyo ameikabidhi kwenye sherehe ya Mahafali ya Kidato cha Nne 2019 Shule ya Sekondari Mufumbu iliyofanyika Tarehe 17.November 2019. Sambamba na hilo Mhe. Sima amekabidhi Mifuko 300 ya Saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kisaki.

"Niwaombe wadogo zangu, wanangu na hususani wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mufumbu vidato vyote someni kwa bidii na msome kwelikweli kwani Elimu kwasasa haina Mbadala na tusitanie kwenye hili, lakini pia niwatake Walimu kuhakikisha mnawalea kikamilifu wanafunzi wetu na hilo sio ombi kwani ninyi ni mashahidi Serikali inatoa fedha nyingi za Elimu bila Malipo na kila mwezi shule inapokea fedha za fidia ya ada na Mahitaji mengine mengi, cha zaidi niseme Wazazi tunapaswa kutambua mchango wetu katika Elimu na sio kujirudisha nyuma katika hili, tuache mambo ya siasa kwenye Elimu, ni kweli serikali inatoa fedha lakini haiwezi kukidhi kila haja" alisema Sima.

Aidha Mhe. Sima amewataka Wazazi/Walezi na Walimu kuwa na mahusiano ya karibu ili kumjengea imani mwanafunzi kusikiliza maoni na mafundisho ya pande zote, kwani kutokuwepo na mahusiano hayo kunawafanya wanafunzi kujitenga na kutofanya vizuri katika masomo yao,
Hayo ameyasema wakati akitoa hutuba yake katika mahafali ya Kidato cha nne 2019 katika Shule ya Sekondari Mufumbu.

Kwa upande mwingine Mhe. Sima amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kulipatia Jimbo la Singida Mjini Umeme na Maji jambo ambalo lilikua tatizo sugu katika Jimbo hilo, Mhe. Sima aliendelea kumshukuru Rais kwa kuipatia vifaa vya Maabara Shule ya Sekondari Mufumbu na kuwafanya wanafunzi kujisomea kwa vitendo.

Aidha Mhe. Sima amewashukuru Walimu kwa kuendelea kujituma kuwafundisha wanafunzi maadili mema.


#bazotvnews



Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida