Posts

Showing posts from April, 2021

OFISI YA DC ARUMERU KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WATOA MISAADA YA PASAKA KWA WANANCHI WASIOJIWEZA NA WAZEE

Image
Na Bazil Mjungu - Arusha: Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akishirikiana na Wadau wa Maendeleo Wilayani humo wametoa Msaada wa vyakula na vifaa vya Huduma za kijamii msaada ambao umelenga familia ambazo hazijiwezi hususani katika Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka inayo adhimishwa tarehe 4 April ya kila Mwaka. Wananchi wameishukuru Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Rais Mahiri Mwana Mama Mhe. Samia Suluhu Hassan na kuiomba kuwatazama kwa jicho la pekee Wazee wenye umri wa zaidi ya miaka zaidi ya 60, Wajane na Wagane ambapo wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu. Wakiongea wakati wa hafla ya upokeaji wa misaada ya vyakula na mafuta kwa makundi Maalum ya watu zaidi ya mia sita katika Kata ya Olorien Halmashauri ya Arusha Wilayani Arumeru kwa ajili ya sikukuu ya pasaka, ambapo wamesema makundi maalum ya wazee, wajane na watoto yatima na haswa wanaoishi katika maeneo ya vijijini yamekua yakisahaulika hivyo wanaiomba Serikali kuwaona kwa jicho la tatu. Awali akitoa taarifa ya namna Wi