OFISI YA DC ARUMERU KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WATOA MISAADA YA PASAKA KWA WANANCHI WASIOJIWEZA NA WAZEE
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akishirikiana na Wadau wa Maendeleo Wilayani humo wametoa Msaada wa vyakula na vifaa vya Huduma za kijamii msaada ambao umelenga familia ambazo hazijiwezi hususani katika Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka inayo adhimishwa tarehe 4 April ya kila Mwaka.
Wananchi wameishukuru Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Rais Mahiri Mwana Mama Mhe. Samia Suluhu Hassan na kuiomba kuwatazama kwa jicho la pekee Wazee wenye umri wa zaidi ya miaka zaidi ya 60, Wajane na Wagane ambapo wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu.
Wakiongea wakati wa hafla ya upokeaji wa misaada ya vyakula na mafuta kwa makundi Maalum ya watu zaidi ya mia sita katika Kata ya Olorien Halmashauri ya Arusha Wilayani Arumeru kwa ajili ya sikukuu ya pasaka, ambapo wamesema makundi maalum ya wazee, wajane na watoto yatima na haswa wanaoishi katika maeneo ya vijijini yamekua yakisahaulika hivyo wanaiomba Serikali kuwaona kwa jicho la tatu.
Awali akitoa taarifa ya namna Wilaya ya Arumeru inavyopambana katika kuhudumia Makundi hayo Mkuu wa Wilaya ya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro amesema pamoja ma Serikali kutoa matibabu bure kwa makundi hayo, amewataka wananchi nao kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhakikisha makundi hayo yanapata huduma bora za kijamii.
Kwa upande wao walioungana na Mkuu wa wilaya ya Arumeru katika kufanikisha upatikanaji wa vyakula hivyo akiwemo Nabii Joe wa huduma ya healing Soul kutoka Arumeru wamesema wao kama Kanisa wameguswa na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Wilaya ya kuyafikia Makundi Maalum na kuyahudumia pasipo kujali Itikadi zao.
Akiongea kwa niaba ya Wadau Nabii Joe wa kanisa la healing soul, Mwenyekiti wa kijiji cha olorien
Akasema:
Huu ni mwendelezo wa kazi za kugusa makundi maalum zinazofanywa na kuratibiwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambapo safari hii katika kipindi hiki cha miezi minne tayari alOfisi imewafikia watu zaidi ya elfu tano ambao baadhi yao wamejenga nyumba za gharama nafuu pamoja na kupatiwa pembejeo za kilimo na mahitaji muhimu ya kijamii "Alisema Nabii Joel".
DC Muro amewataka Wananchi kuchukua tahadhari ya kudanganywa na Wanasiasa wanaowarubuni kutokufanya kazi kwa kisingizio Serikali itafanya kila kitu, Wajitokeze kushiriki Miradi ya Serikali na yao Binafsi ili kujiletea Maendeleo.
#bazotvNews
Hongera DC Muro
ReplyDelete