Posts

Showing posts from 2020

MTATURU ATEMBELEA UJENZI WA SHULE YA MSINGI MBWANJIKI NA KUKABIDHI MIFUKO 30 YA SARUJI

Image
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu leo 15/12/2020 Ametembelea ujenzi wa Shule ya Msingi Mbwanjiki na Kukabidhi Mifuko 30 ya Saruji. Mtaturu Amekabidhi Saruji hiyo baada ya Shule hiyo kukwama ujenzi wake kwa zaidi ya Miaka 30 iliyopita Shule hiyo ikikamilika itaondoa changamoto ya Wanafunzi kutembea umbali Mrefu na msongamano katika Shule wanazosoma za Ikungi, Ighuka na Matongo.

DIWANI PEKEE WA KATA YA NTUNTU AMBAYE NI MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA IKUNGI NA MJUMBE WA BARAZA KUU CHADEMA TAIFA ALA KIAPO CHA UDIWANI

Image
Diwani pekee wa Kata ya Ntuntu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Ikungi na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa Ndg. Omary Athumani Toto Ameapa mbele ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ikungi kuwa Diwani wa Kata hiyo licha ya Halmashauri Kuu ya chama chake kuweka zuio la wanachama wote waliochaguliwa kutokula kiapo kwa kuwa chama hicho hakijakubaliana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu Mwaka 2020 na kuwa hawawatambui viongozi waliochaguliwa akiwepo Rais John Magufuli. Mhe. Omary Athumani Toto akipokea Ilani ya CCM kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt Rehema Nchimbi.

MTATURU ATOA MILIONI 1. UNUNUZI WA VYEREHANI VITANO CHUO CHA RYADHA CHA KIISLAM IKUNGI

Image
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe Miraji Mtaturu leo 12/12/2020 Amehudhuria Kufungwa kwa Chuo Cha Kiislam Cha Ryadha Cha Ikungi Mkoani Singida na Kukabidhi Milioni 1 kwaajili ya Ununuzi wa Vyerehani vya kujifunzia Wanafunzi Chuoni hapo. #ManenoKidogoKazizaidi

MTATURU ATEKELEZA AHADI YA KUMPATIA BAISKELI MWALIMU ELIAS MKUKI (MLEMAVU) WA MUGHUMBU NTUNTU

Image
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Adam Mwiru Amemkabidhi Baiskeli Mwalimu wa kujitolea katika shule ya Msingi Mughumbu iliyopo Kata ya Ntuntu Mwl. Elias Mkuki ambaye ni Mlemavu wa Viungo ili imsaidie kufika Shuleni kwa wakati Baiskel hiyo imekua ni sehemu kutekeleza ahadi ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Miraji Mtaturu aliyowahi kuitoa kwake. Msaada huo ameutoa pia ili kuwaenzi watu wenye Ulemavu ambapo Disemba 03/2020 ilikuwa ni Maadhimisho ya siku ya watu wenye Ulemavu Duniani. Akipokea Baiskel hiyo Mwl. Elias Mkuki amesema "Kwakweli nimejawana furaha kubwa mno Moyoni mwangu, aliniahidi siku zahivi karibuni kuwa ataniletea Baiskeli ninamshukuru nimeioata, Lakini niseme tu kwamba kuna viongozi wengi huwa wana ahidi Wananchi na hata walemavu Kama Mimi lakini hawatekelezi kwakweli Mungu amlinde Mtaturu katika Utumishi wake" alisema Mwl. Elias. #bazotvNewsUpdate.

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

Image
        Rehema Sombi Omary Mgombea UBUNGE VITI MAALUMU UVCCM kutoka Mkoa wa Singida. *WASIFU BINAFSI* *JINA KAMILI*: REHEMA SOMBI OMARY Jinsia:Ke Uraia :Mtanzania Kuzaliwa:07,March 1994 Lugha:Swahili,Kiingereza Anuani:S.L.P 809, Singida,Tanzania Barua Pepe : omaryrehema31@gmail.com *ELIMU* - Shahada ya Sayansi katika Uuguzi -Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana-Shahada ya Uuguzi -Bwiru Girls high School-Cheti cha Elimu ya Sekondari ya juu -Kipata Girls Islamic High School-Cheti cha Elimu ya Sekondari -Utemini Primary School-Cheti Cha Elimu ya Msingi   -Ummu Salama nursery school- Cheti Cha elimu ya awali *UZOEFU KITAALUMA* -Afisa Muuguzi kitengo cha ICU/CCU hospital ya Benjamin Mkapa-Dodoma (2019-2020)  -Mafunzo Tarajali katika hospital ya The Benjamin Mkapa-Dodoma (2018-2019) -Mafunzo kwa vitendo hospital ya Rufaa ya Dodoma( 2016-2017) -Mafunzo kwa vitendo hospital ya Rufaa ya Singida (2015-2016) -Mafunzo kwa vitendo kituo cha afya Makole-Dodoma (2014-2015)   *UZOEFU WA UONGOZI KITAAL

MTATURU ASHIRIKI UJENZI WA UPANUZI WA IKULU CHAMWINO - DODOMA

Image
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu leo tarehe 12/07/2029 ameshiriki Ujenzi wa Upanuzi wa Ikulu ya Chamwino - Dodoma.

MTATURU AMEFIKA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA KUMUONA MGONJWA ALIYE MSAFIRISHA KUTOKA KIPUMBWIKO KUJA KUTIBIWA HAPO NA YEYE KUGHARAMIA MATIBABU YAKE

Image
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu amefika Hospital ya Benjamini Mkapa kumuona Mgonjwa Bi. Elizabeth Lissu aliyemsafirisha kutoka Kipumbwiko Ikungi kuja kupatiwa matibabu baada ya Mbunge kujulishwa kuwa Mama huyo amepooza miguu na yupo kitandani zaidi ya Mwaka bila kupatiwa matibabu. Mhe. Mtaturu amekubali kugharimia Matibabu ya bi Elizabeth Lissu na madaktari wameeleza atafanyiwa kipimo cha MRI.

VIJANA 52 KUTOKA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA WAHAMIA CHAMA CHA MAPINDUZI IKUNGI

Image
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi Ndg. Mika Likapakapa amepokea  Vijana 52 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA walioamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kwa kile walichodai kuwa wamechoshwa na tabia za chama hicho za kuwalazimisha kuwakataa hata wazazi wao kisa wako CCM, Vijana hao wamedai kufurahishwa na Utendaji kazi za Maendeleo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa kipindi kifupi cha Miezi 9 tangu kuapishwa Bungeni September 3/2019.

Mhe. MTATURU NA TISA YA UTUMISHI.

Image
Na Koti la Kung'aa. Brazili ni nchi pekee duniani iliyowahi kuishikilia historia ya soka la dunia kwa muda mrefu sana na vijana wengi walikuwa wanatamani kupata fursa ya kumiliki hata chembe ya uwezo wa aliyekuwa mmoja wa Icon ya soka la Brazil kati ya Carlos Dunga na kina Ronaldo De Lima katika kulisakata Samba (Soka la Kibrazili) Kitu pekee kilichowahi kumbeba Ronaldo De Lima, nguli huyu aliyekabidhiwa jezi nambari 9 ni ufundi,ubunifu na matumizi ya maarifa ya ziada katika kuhakikisha timu inapata matokeo yenye furaha kwa wabrazili na wafuasi wa soka la Brazili. Hoja yangu sio soka la Brazili na wababe wake bali ni * UBUNIFU ,MAARIFA,USHAWISHI NA UFUNDI * katika jimbo la Singida mashariki ambalo mpaka makala hii inaenda kwenye tanakilishi lilikuwa linaongozwa na Mheshimiwa Miraji J. Mtaturu aliyetumia miezi tisa tu kupambana na changamoto za wananchi kupitia nafasi yake kama mbunge. Kimahesabu Mheshimiwa Mtaturu amekaa ofisini (Kama mbunge)kwa sekunde 388800 ambazo ni sawa

MTATURU ADHAMINI UJENZI WA MABANDA YA KUPUMZIKIA ABIRIA STENDI MPYA IKUNGI

Image
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu Leo tarehe 06/06/2020 amekabidhi Mabanda ya Kupumzikia Abiria na Akina Mama wajasiriamali Stendi ya Mabasi Ikungi yenye thamani ya Tsh 3,958,000/= Mabanda hayo yamezinduliwa na Mhe. Edward Mpogolo. Mkuu wa Wilaya ya Ikungi.

MTATURU AKUTANA NA BODABODA JIMBONI KWAKE KUSIKILIZA KERO NA KUZIPATIA UFUMBUZI

Image
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe Miraji Mtaturu leo Tarehe 31/05/2020 amekutana na Bodaboda wa Wilaya ya Ikungi ikiwa ni utaratibu wake wa kawaida kukutana na Makundi mbalimbali ili kupokea kero na changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi. #MtaturuJimboni

CHADEMA YAZIDI KUPUKUTIKA SINGIDA

Image
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Singida ndugu Shabani Limu Amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) rasmi leo 30/5/2020 nakukabidhi kadi ya chadema kwa Mhe. Munde Tambwe Abdallah (Mb)  Mjumbe wa Kamati kuu na mlezi wa CCM Mkoa Singida. #Ccm #Chaguolao

JENGO LA UPELELEZI KITUO CHA POLISI WILAYA YA IKUNGI KUKAMILIKA

Image
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu leo 30/05/2020 amekabidhi mifuko ya Saruji ili nisaidie kumalizia Ujenzi wa Jengo la Upelelezi Kituo cha Polisi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida. #Mtaturukazini

HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI YAENDELEA KUPATA HATI SAFI

Image
Mweyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe Ally Juma Mwanga amewapongeza watumishi wa Halmashauri hiyo chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ndugu Justice Lawrence Kijazi kwa kuendelea kusimamia ukusanyaji mapato na kuongeza Mapato katika Wilaya hiyo. #bazotvUpdate

ZIARA YA WAZIRI MEDARD KALEMANI SINGIDA MASHARIKI YALETA FARAJA KWA WANANCHI

Image
Baada ya Ziara ya Waziri Dkt Medard Kalemani Aprili 18, 2020 aliagiza Kijiji cha Kimbwi kuwekewa Umeme Ndani ya Siku 30 Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu Tarehe 17/05/2020 amefika kukagua mradi huo na nguzo 152 zimesimikwa, Wananchi wafurahia. #ManenokidogokaziZaidi #SindigaMasharikiMaendeleo

UTEKELEZAJI WA OMBI LA MBUNGE MTATURU WIZARA YA MAJI UNAENDELEA

Image
Baada ya mvua kusimama na Ardhi kuwa kavu hatimae Mkandarasi Target amefika Kijiji cha Sakaa kumalizia kuchimba kisima kirefu na Tarehe 17/05/2020 yamepatikana Maji Safi na baridi kwa Ajili ya Matumizi ya Wananchi, Vijiji vya Msuke, Mkunguwakihendo, Mampando, Msule na Ujaire vinafuatia. #ManenokidogokaziZaidi #SingidaMasharikiMaendeleo

MTATURU AWASILISHA KILIO CHA WASTAAFU:

Image
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe Miraji Mtaturu amedai kuwa baadhi ya wastaafu wanashindwa kulipwa fedha zao kwa wakati na hivyo kuomba wasaidiwe kupata stahiki hizo kwani wametumikia vyema nchi hii. Mtaturu amesema hayo wakati akichangia mapitio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2020/21 ambapo ametolea mifano wa wazee wawili Gamaliel Mathia Masawe wa Makiungu na Mohammed Selemani Ntandu wa Unyahati wote wa jimboni kwake ambao hawajapata stahiki hizo kwa miezi saba.

SHANTA MINING COMPANY LTD YAIKABIDHI WILAYA YA IKUNGI VIFAA VYA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA VYENYE THAMANI YA. 2.2 MILIONI

Image
   Na Bazil Mjungu: Ikungi - Singida Kampuni ya Uchimbaji Madini - Shanta Mining Company Limited ya Mkoani Singida, Imemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi msaada wa Vifaa vya Kujikinga na Virusi vya Corona vyenye Thamani zaidi ya Milioni 2.2 kuunga mkono juhudi za Mhe Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha ugonjwa wa Corona hauenei Nchini.   Akikabidhi msaada huo,  kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,  Ndug Justice Lawrence Kijazi,  jana April 24 / 2020 kwa niaba ya Kampuni hiyo Eng. Philbert Rweyemamu Meneja Mkuu,  Meneja huyo amesema kampuni yao imetoa msaada huo wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona,  ikiwa ni kushiriki moja kwa moja kwa vitendo ili kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli. Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Eng. Philbert Rweyemamu amesema pamoja na vifaa hivyo walivyotoa,  Kampuni ya Shanta Mining Limited Imekabidhi hivi karibuni Tsh Milioni 100 kwenye m

UWT UKEREWE KUSAKA KURA ZA RAIS DKT MAGUFULI, MBUNGE NA MADIWANI KUPATA USHINDI WA KISHINDO

Image
Na Peter Fabian Ukerewe. Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wa Wilaya ya Ukerewe wameahidi kumuunga mkona Mwenyekiti wa CCM taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kushinda kwa kishindo uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu 2020. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa UWT Wilaya hiyo Spelancia Nagabona wakati wa hafla ya kupokea Baiskeli 59 za wenyeviti na makatibu wa Jumuiya hiyo wa Kata 25 za Jimbo la Wilaya ya Ukerewe zilizotolewa na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Mwanza Kemilembe Lwota na kukabidhiwa mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la UWT Wilaya. Mwenyekiti Nagabona aliwaeleza wajumbe wa Baraza hilo kuwa baiskeli hizo zitakabidhiwa kwa kila Mwenyekiti na katibu wa Jumuiya hiyo wa Kata zote 25 ili kuwasaidia usafiri wa kuwafikia wanachama wa ngazi za matawi na kuhamasisha wananchi ili kuwachagua wagombea watakaopitishwa na CCM kugombea Ubunge na Udiwani huku wakihakikisha wanampigia debe Rais Dkt Magufuli achaguliwe t