SHANTA MINING COMPANY LTD YAIKABIDHI WILAYA YA IKUNGI VIFAA VYA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA VYENYE THAMANI YA. 2.2 MILIONI


   Na Bazil Mjungu: Ikungi - Singida

Kampuni ya Uchimbaji Madini - Shanta Mining Company Limited ya Mkoani Singida, Imemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi msaada wa Vifaa vya Kujikinga na Virusi vya Corona vyenye Thamani zaidi ya Milioni 2.2 kuunga mkono juhudi za Mhe Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha ugonjwa wa Corona hauenei Nchini.


  Akikabidhi msaada huo,  kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,  Ndug Justice Lawrence Kijazi,  jana April 24 / 2020 kwa niaba ya Kampuni hiyo Eng. Philbert Rweyemamu Meneja Mkuu,  Meneja huyo amesema kampuni yao imetoa msaada huo wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona,  ikiwa ni kushiriki moja kwa moja kwa vitendo ili kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli.


Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Eng. Philbert Rweyemamu amesema pamoja na vifaa hivyo walivyotoa,  Kampuni ya Shanta Mining Limited Imekabidhi hivi karibuni Tsh Milioni 100 kwenye mfuko wa Maafa wa Waziri Mkuu.


Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Mask box 10,  Chemical Suit 20,  Gloves box 85,  Pressure sprays 5 na Sanitizer lita 15.
Eng. Philbert Rweyemamu amesema kampuni yao haitasita kutoa mchango wake kwa jamii kwani bila kushirikiana na jamii kampuni yeyote haiwezi kusonga mbele.


“Kama nilivyosema tuna janga hili kubwa,  Janga hili la maradhi ya Corona haliko tu Tanzania lakini lipo sehemu zote za dunia na kama sote tunavyojua ugonjwa huu hauna tiba, tiba pekee ni kujihami usikupate nawewe kusaidia wengine wasiupate" (Alisema Eng. Philbert Rweyemamu)

“Mheshimiwa Rais wetu Machi 22 Mwaka huu, katika hotuba yake kwa taifa kuhusu janga hili, akitangaza maradhi ya Corona alitupa tahadhari , alituambia pamoja na kuchapa kazi na kuendelea na shughuli zetu za kila siku za kutafuta riziki lazima tuchukue tahadhari kwa kunawa mikono, kutokusanyika na lakini na kutoacha kumuomba Mungu" (Aliendelea kusema Eng. Philbert Rweyemamu)


“Hivi sasa ni wazi kwamba tahadhari hizo inabidi tuzizingatie kuliko ilivyokua mwanzo tena kupitia watumishi wa Afya Ndugu Mkurugenzi waende kutoa elimu vijijini huko jinsi ya kujikinga na kuwaelekeza jinsi ya kuvaa hizi Barakoa,  kingine niongeze kuwa nivizuri vifaa hivi vikawafikia na wananchi zisibaki tu kwa watumishi wa Umma itakua hamjatenda sawa. (Alisema Eng. Philbert Rweyemamu)


Eng. Philbert Rweyemamu Ameongeza kuwa  alizungumza na madktari baadhi na wakamwambia kuwa  ni vema kuvaa barakoa wakati unakwenda kwenye msongamano wa watu lakini pia watu wanaweza kutengeneza wenyewe si lazima kununua madukani.


Pamoja na mambo mengine, Eng. Philbert Rweyemamu ametoa wito kwa wadau na Makampuni mbalimbali Nchini kuisaidia serikali kwa kutoa msaada wa vifaa vya kupambana na corona akitolea mfano kwa nchi nyingine wafanyabiashara walivyosaidia nchi zao.


Akipokea msada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,  Ndug Justice Lawrence Kijazi, amesema kwa niaba ya Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,  amethibitisha na kupokea msaada huo wa vifaa vya kujikinga na Maambukizi ya Covid-19,  kutoka kwa kampuni ya Shanta Mining Limited na watahakikisha vinatumika kama maelekezo ya Wizara ya Afya inavoelekeza na atahakikisha watumishi wa afya wanaenda kuwafikia Wananchi ili kuwapatia elimu ya Kujikinga na ya matumizi ya vifaa hivyo.


"Niseme tu sisi Watumishi wa Mhe. Rais tupo msitari wa Mbele kuhakikisha tunawaelekeza wananchi kufuata taratibu na maelekezi ya wizara ya Afya ili kuepukana na maambukizi haya ya Covid-19. (Alisema Kijazi).


Aidha Ndugu Justice Kijazi ameongeza kuwa watumishi wa Afya na idara zingine zilishapata mafunzo maalum ya kutoa elimu kwa wananchi hivyo amewaasa kufanya yale waliyoelekeza na si vinginevyo.


Nae Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt Vitalis Katalyaba amekiri kupokea vifaa hivyo na kahidi kuwa vitatumika kama maelekezo yalivyotoka.



#Bazotvonline:
 

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida