Posts

Showing posts from May, 2021

MTATURU AIOMBA SERIKALI KUANZISHA MAMLAKA YA MAJI MJI WA IKUNGI

Image
Na Bazil Mjungu: Dodoma MBUNGE wa Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu ametaja mambo manne ya kuzingatiwa katika kuhakikisha hali ya upatikanaji maji katika wilaya ya Ikungi inakuwa ya kuimarika ikiwemo kuhakikisha vijiji kumi vinapata chanzo cha maji cha uhakika. Akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji Mei 7 bungeni ametaja vijiji hivyo kuwa ni Ntuntu, Taru, Mbogho, Mwau, Mahambe, Choda, Manjaru, Tumaini, Matongo na Unyakhanya. “Nikupongeze Waziri na timu yako kwa kazi nzuri mnayoifanya katika kuhakikisha wananchi wanapata maji,na Ilani yetu ya Uchaguzi ya CCM katika ukurasa wa saba Ibara 9 D kifungu cha kwanza imeeleza wazi katika miaka mitano kuwa itaongeza nguvu katika upatikanaji wa maji, “Hivyo katika hili kasi inatakiwa iendelee kuongezeka katika kuwekeza zaidi, najua kazi imefanyika na mimi nina ushahidi katika jimbo langu au Wilaya ya Ikungi tumepata bilioni 3.7 kwa mwaka uliopita,safari hii naona wametubana sana kwa wilaya nzima tumepata Bilioni 1.7 ,maa

BILIONI SITA ZIMETENGWA KWA AJILI YA MAADALIZI YA BARABARA KUTOKA SINGIDA HADI TANGA

SERIKALI imeahidi kuijenga kwa awamu barabara ya Handeni – Kiberashi –Kwamtoro hadi Singida yenye Kilomita 641 kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. Ahadi hiyo imetolewa Mei 5 bungeni na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Leonard Chamuriho wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu. Katika swali lake mbunge huyo ameihoji serikali ni lini itajenga barabara hiyo ambayo ina manufaa kwa mikoa minne. “Barabara hii tuna maslahi nayo , inaunganisha mikoa minne,ina historia katika nchi yetu na imefika sasa wakati serikali iamue kuijenga iishe kuliko kuanza kuwa na vipande vidogo vidogo,Je ni lini serikali itaanza kujenga barabara yote,?”.alihoji Mtaturu. Akijibu swali hilo Mhandisi Chamuriho amesema kwa sasa wanaendelea kuijenga barabara hiyo kwa vipande kulingana na upatikanaji wa fedha. “Mwaka huu barabara hii imezingatiwa na tutajenga kipande kimoja na tutaendelea kuijenga kwa kulingana na upatikanaji wa fedha ,”.alisisitiza. Awali akijibu swali la mbung