UWT UKEREWE KUSAKA KURA ZA RAIS DKT MAGUFULI, MBUNGE NA MADIWANI KUPATA USHINDI WA KISHINDO

Na Peter Fabian Ukerewe.

Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wa Wilaya ya Ukerewe wameahidi kumuunga mkona Mwenyekiti wa CCM taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kushinda kwa kishindo uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu 2020.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa UWT Wilaya hiyo Spelancia Nagabona wakati wa hafla ya kupokea Baiskeli 59 za wenyeviti na makatibu wa Jumuiya hiyo wa Kata 25 za Jimbo la Wilaya ya Ukerewe zilizotolewa na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Mwanza Kemilembe Lwota na kukabidhiwa mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la UWT Wilaya.

Mwenyekiti Nagabona aliwaeleza wajumbe wa Baraza hilo kuwa baiskeli hizo zitakabidhiwa kwa kila Mwenyekiti na katibu wa Jumuiya hiyo wa Kata zote 25 ili kuwasaidia usafiri wa kuwafikia wanachama wa ngazi za matawi na kuhamasisha wananchi ili kuwachagua wagombea watakaopitishwa na CCM kugombea Ubunge na Udiwani huku wakihakikisha wanampigia debe Rais Dkt Magufuli achaguliwe tena kuliongoza taifa kwa miaka mitano mingine tena.

Alieleza kuwa Rais Dkt Magufuli amitekeleza ahadi ya majisafi na kuboresha vituo vya afya na Hosptali ya Wilaya vinatoa huduma bora kwa wananchi sanjari na kuimalisha usafiri ndani ya ziwa Victoria hudusani kisiwa kikubwa cha Ukerewe na Ukara pia kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi wanapata elimu bure ikiwemo sekondari hivyo nijambo la kujivunia kumchagua tena Rais na wawakilishi wa wananchi ambao ni Mbunge na Madiwani wa CCM bila shaka yoyote.

Nagabona alisema wananchi wa Wilaya ya Ukerewe walifanya ushabiki na wakakosea kuuchagua upinzani kwa miaka nane ambapo mambo yalikuwa hayaendi kabla ya Mbunge Joseph Mkundi aliyekuwa Chama cha Chama kusoma alama za nyakati na kurejea CCM kwa kuwa alijua jeshi kubwa la wanawake wa Wilaya ya Ukerewe limejipanga kurejesha Jimbo kutoka upinzani hata hivyo tumejipanga kuhakikisha vitongoji, vijiji, Kata, Jimbo na Rais wote wanatoka CCM kwa ushindi wa kishindo.

"Nikupongeze Mbunge Lwota kwa kutekeleza ahadi yako yakutusaidia usafiri ili kuhakikisha kazi za Jumuiya zinaimalika na kuwafikia wanachama ikiwemo kuongeza wanachama wapya wa Jumuiya yetu na Chama lakini pia kuisemea miradi mbalimbali iliyotekelezwa na serikali kupitia Ilani ya Uchaguzi na ahadi za viongozi ikiwemo wabunge na madiwani," alisema.

Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Mwanza, Kemilembe Lwota akikabidhi baiskeli hizo alisema ametekeleza ahadi ya kutoa usafiri kwa viongozi wa Jumuiya hiyo ngazi ya Kata katika Wilaya zote ambazo Jografia za kuwafikia wanachama zinakabiliwa na  inachangamoto ya usafiri.

"Niliwaahidi kupitia kikao cha Baraza Kuu la Jumuiya Mkoa leo nimekabidhi baiskeli 59 kwa ajili ya matumizi ya usafiri lakini pia nimetoa mabati 100, mbao 100 na mifuko 50 ya saruji ili kukamilishwa kwa mradi wa ujenzi wa jengo la kitegauchumi la Jumuiya Wilaya ya Ukerewe ili kujiingizia fedha zitakazosaidia kuendeleza Jumuiya pia nimetoa mashuka 200 na vitanda Jumuiya Hospitali ya Wilaya iliyopo Mji wa Nansio sanjali na kuipatia Jumuiya mradi wa pikipiki kuwasaidia kuingiza fedha za uendeshaji shughuli za kila siku," alisema Lwota.

Mbuge Lwota amewahakikishia wanachama wa CCM, Jumuiya hiyo na wananchi kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli mzalendo utaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhakikisha huduma bora zinapatikana kupitia sekta zote hiyo waendelee kuiunga mkono CCM na serikali kufika malengo na taifa liweze kufikia uchumi wa kati na upatikanaji huduma bora za kijamii.

"Wanawake ni jeshi kubwa hivyo tujipange sawa sawa kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ili kuendelea kuongoza taifa na kuhakikisha raslimali za taifa zinawanufaisha watanzania wote na kupatikana maendeleo yatakayoambatana na huduma bora za kijamii chini ya Rais Dkt Magufuli inawezekana na mumemuona mzalendo amekuwa akipambana kutekeleza miradi mikubwa kwa fedha za kodi yetu," alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo, Ally Mambile alimpongeza Mbunge Lwota kwa kujitolea kusaidia baiskeli ambazo watazitumia kwa usafiri lengo ikiwa ni kutafuta kura za wagombea wa CCM mwezi Oktoba lakini pia zitawezesha jeshi kubwa la wanawake kufika maeneo mbalimbali kuwafikia wananchi na kuwaomba wawamchague Rais Dkt Magufuli, Wabunge na Madiwani.

"Niwahase viongozi wa UWT Wilaya na Kata kuzitumia baiskeli hizi kuhakikisha malengo yanafikiwa ikiwemo kuongeza wanachama na kupata ushindi wa kimbunga zaidi ya uhuu wa serikali za Mitaa ambapo tumefanya vizuri na kauli mbiu yetu Wilaya ya Ukerewe ni CCM 2020 ni Rais Dkt Magufuli, Mbunge na Madiwani Kata zote 25 mali ya CCM," alisema.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Boniphace 
Magembe aliwahakikishia viongozi na wanachama wa CCM kuwa serikali imejipanga kuhakikisha amani na utulivu wakati wa michakato ya kura za maoni na kampeni za Uchaguzi mkuu kwa wagombea kunadi sera zinafanyika bila vurugu na watakaoleta uchochezi na uvunjifu wa amani watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na hawata mfumbia macho mtu ama kikundi cha watu wachache watakaoandaliwa kuvuruga amani maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Ukerewe, Joseph Mkundi (CCM), aliwashukuru viongozi na wanachama kumpokea alipoamua kurejea CCM na kuwa bega kwa bega kuhakikisha maendeleo yanapatikana ikiwemo kutekelezwa kwa miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta za majisafi, elimu, barabara, umeme, kilimo cha kisasa, ufugaji wa tija, usafiri kulingana na jiografia ya visiwa vyetu hivyo tuhakikishe Rais Dkt Magufuli anapeta kwa kishindo kikubwa.

#bazotvonline

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida