Mhe. MTATURU NA TISA YA UTUMISHI.


Na Koti la Kung'aa.

Brazili ni nchi pekee duniani iliyowahi kuishikilia historia ya soka la dunia kwa muda mrefu sana na vijana wengi walikuwa wanatamani kupata fursa ya kumiliki hata chembe ya uwezo wa aliyekuwa mmoja wa Icon ya soka la Brazil kati ya Carlos Dunga na kina Ronaldo De Lima katika kulisakata Samba (Soka la Kibrazili)

Kitu pekee kilichowahi kumbeba Ronaldo De Lima, nguli huyu aliyekabidhiwa jezi nambari 9 ni ufundi,ubunifu na matumizi ya maarifa ya ziada katika kuhakikisha timu inapata matokeo yenye furaha kwa wabrazili na wafuasi wa soka la Brazili.

Hoja yangu sio soka la Brazili na wababe wake bali ni *UBUNIFU ,MAARIFA,USHAWISHI NA UFUNDI* katika jimbo la Singida mashariki ambalo mpaka makala hii inaenda kwenye tanakilishi lilikuwa linaongozwa na Mheshimiwa Miraji J. Mtaturu aliyetumia miezi tisa tu kupambana na changamoto za wananchi kupitia nafasi yake kama mbunge.

Kimahesabu Mheshimiwa Mtaturu amekaa ofisini (Kama mbunge)kwa sekunde 388800 ambazo ni sawa na masaa 6480 na ni sawa na siku 270 au wiki 39 lakini ubunifu na utundu alioutumia katika kuhakikisha jimbo la Singida mashariki linakaa kwenye ramani si wa kupuuzwa ama wa kuchukuliwa kiwepesi fanyeni ulinganishaji yakinifu.

Kwa muda wa miezi tisa ya utumishi wake amebuni, kutekeleza jumla ya miradi yenye thamani ya 8billion(Hapa sijaiweka 6billions fedha zilizotengwa wa ajili ujenzi wa barabara ya lami kutoka njiapanda-Kwa mtoro-Handeni kwa kiwango cha lami)iliyotengwa kujenga barabara kutokeajimboni ili kuchochea maendeleo ambayo ni wastani wa miradi/changamoto 8 kwa wiki Zilikuwa zinashughulikiwa, Na ndani ya miezi 9 ameweza kushughulikia changamoto ya maji,umeme,barabara, Afya ,Uchumi kupitia vikundi na mwelekeo wa jimbo si wa kutia shaka kabisa.

Ndugu zangu, Ikiwa utaamua kusimama na huyu mheshimiwa ndani na nje ya chama sikushauri uende na matokeo yako unaweza ukatoka na kiharusi siku ya kura za maoni/ uchaguzi wenyewe kwasababu ikiwa amekiletea chama heshima ndani ya miezi tisa kwa kiwango hiki unadhani utashinda kwa hoja zipi dhidi ya matendo yake ya kibunge yanayoonekana kwa wananchi?

Mheshimiwa Mtaturu angekuwa ametumia miaka mitano katika utumishi wake sijui tungekuwa wapi kimaendeleo kwasababu mpaka sasa ametumia tisa moja tu kati ya tisa saba zilizopo kwenye miaka mitano na maendeleo yanaonekana barabara kabisa, Vuta picha kidogo.....

USHAURI WANGU: Tuko kwenye wakati muafaka wa kupractice democracy ya nchi yetu lakini kwa ubunifu, maarifa,ushawishi na umakini uliomo katika Mheshimiwa Mtaturu ni vyema apewe tisa zingine zinazoanzia 2020-2025 ili tutumie fikra na maono yake aliyoyaanzisha kufikia Mashariki ya kisasa zaidi.
TUNA TISA NYINGI ZENYE MAENDELEO KUPITIA MTATURU.

Na
Koti la Kung'aa
Kikio,
Singida Mashariki

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida