CHIFU SINGU MISSANGA ASIMIKWA KUWA KIONGOZI WA KABILA LA WANYATURU
Leo Tarehe 17/11/2021 imekuwa baraka Ihanja Wilayani Ikungi Mkoani Singida Amesimikwa rasmi Chifu Singu Missanga Senge Kuwa kiongozi wa Utemi wa UNYIKUNGU katika kabila la Wanyanturu.
Hafla hii ya usimikwaji ilianza kwa Dua Maalum ilioyo ongozwa na Viongozi wa Dini Shekhe, Mchungaji na Viongozi wa Kimila ya Kknyaturu.
Chifu Singu Missanga amesimikwa na Baraza la Wazee la ukoo wa Chifu Missanga Senge katika kabila la Wanyaturu na kushuhudiwa na Chifu Mkuu wa Ikungi Abraham Gwau.
Akimwakilisha Jerry Muro Mkuu wa wilaya wa Ikungi, Katibu Tawala Wilaya Ndg. Dijovison Ntangeki amesisitiza Viongozi wa Kimila kuwa ndio nguzo ya Amani na uwajibikaji hivyo watumie nafasi hizo kusaidia kuelelimisha jamii kuacha Mila potofu, kuhamasisha jamii kuenzi mila na tamaduni za Tanzania. Ikiwemo uhamasishaji upendo, maridhiano, umoja na mshikamano wa taifa ikienda sambamba na kulingania tunu za taifa pamoja na upendo ili kuondoa ukiukwaji wa Hali za binadamu wenye vionjo vya ubaguzi pia utunzaji wa mazingira ya asili, upandaji miti kwa wingi,kuhamasisha shughuli, za maendeleo , kilimo , ufugaji na uchapa kazi
Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo Ni Afisa Tarafa wa kijiji cha Ihanja , Whe. Madiwani, wenyeviti serikali ya vijiji na watendaji wa kata zote .
Ushauri na Mapendekezo
0766430685 WhatsApp.
#bazotvnews
Comments
Post a Comment