SINGIDA: BARAZA LA MADIWANI IKUNGI LAZITAKA KAMPUNI ZILIZONUNUA PAMBA KWA WANANCHI KUWALIPA FEDHA ZAO KABLA YA NOVEMBA 30/2019
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
limezitaka Kampuni zilizonunua Pamba kwa wakulima wilayani humo
kuwalipa mara moja wakulima fedha wanazo dai kabla ya mwisho wa mwezi novemba 2019
kwani msimu wa kilimo umefika watashindwa kuandaa mashamba yao kama watakua hawajalipwa fedha hizo.
Akiongea kwenye Baraza lililofanyika tarehe 13.11.2019 Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Diwani wa Kata ya Mtunduru
Mhe. Ramadhani Mpaki ameitaka Kampuni ya ununuzi Pamba ya Biosustain kufanya hivo mapema
ili kutowakatisha tamaa wakulima kuendelea na kilimo hicho,
kwa upande wake Makamu Mwenyeketi wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Issuna Mhe. Missai amewataka wakulima
kuandaa mashamba yao mapema ili kuwahi msimu wa mvua unatotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Nae Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Justice Lawrence Kijazi
amewahakikishia wakulima kulipwa fedha zao kwani atafuatilia kwa ukaribu maagizo ya Baraza.
Swala la kulipwa fedha wakulima
Lilijiri baada ya Madiwani kuleta sintofahamu kwenye kikao cha baraza walipotoa hoja ya malalamiko yao kuhusu wakulima kucheleweshewa fedha zao na wanunuzi wa Pamba.
Na,
#bazilmjungu
Comments
Post a Comment