MTATURU ATAHADHARISHA KANUNI ZA SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI.

Na Bazil Mjungu Dodoma:
MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki (CCM), Mhe. Miraji Mtaturu, ametahadharisha kanuni zitakazotungwa kwenye muswada wa sheria ya Ulinzi wa taarifa binafsi wa mwaka 2022  kuhakikisha zinaendana na sheria ili zisiibue malalamiko kwa wananchi.

Akichangia leo bungeni, Mtaturu amesema sheria hiyo ni nzuri lakini utungaji wa kanuni hizo uendane na sheria iliyopitishwa.



Pamoja na sheria hii kuwa nzuri na tumekuwa tukipitisha hapa, kumekuwa na changamoto ya kanuni, niombe sana kwenye eneo hili na sisi tunamuamini Waziri, sheria ikitungwa nzuri iende hivyo hivyo na kanuni ziwe nzuri,”amesema Mtaturu.

Mtaturu amesema eneo la utungaji wa kanuni linaweza kuwa mwiba mwingine katika utekelezaji wa sheria zinazopitishwa na bunge.



Tumekuwa tukipitisha baadhi ya sheria lakini ile nafasi ya kutengeneza kanuni huwa inakwenda kuharibu kabisa sheria, matokeo yake wabunge tunaulizwa mlipitishaji sheria hii, kumbe kanuni imekwenda kuharibu kabisa maudhui mazima ya sheria ambayo tumepitisha hapa,” amesema Mtaturu.


Aidha Mhe Mtaturu Amemuomba Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta Tulia Ackson kuomba kanuni zipelekwe Bungeni ili wajiridhishe kabla hazijaanza kutumika.

Kuhusu Muswada wa Sheria ya Uwekezaji Tanzania wa Mwaka 2022, amesema utaongeza wawekezaji nchini na kuongeza wigo wa ajira.

“Wawekezaji wengi walikuwa wanasita kuwekeza, leo hii wamekuwa na mahitaji ya kuona dhamira ya serikali yetu katika eneo la uwekezaji, hii imejenga imani zaidi kwa wawekezaji,”amesema.


Kwa upande mwingine Mhe. Mtaturu ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuja na sheria hiyo.

"Hii sheria tumeisubiri kwa muda mrefu,niishukuru na kuipongeza serikali kwa usikivu wake,kwa kusikiliza kilio cha wadau na kuja na sheria hii,"amesema Mtaturu.

#mtaturubungeni
#bungenidodoma
#jimbosingidamashariki

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida