DARASA NA STREETLECTURE UTAJIRI na UMASIKINI
Mfano: Mtu anayeshinda bahati nasibu au kamari. Hata akishinda milioni 100 si tajiri: Ni maskini mwenye pesa nyingi. Ndiyo sababu 90% ya mamilionea wa bahati nasibu wanakuwa maskini tena baada ya miaka 5.
Pia una matajiri ambao hawana pesa.
Mfano:Wajasiriamali wengi.
TAYARI wapo njiani kuelekea kwenye utajiri japokuwa hawana pesa, maana wanakuza akili zao za fedha na huo ndio utajiri.
*Tajiri na maskini wanatofauti gani?*
Kwa maneno rahisi: Tajiri anaweza kufa ili kuwa tajiri na hutumia mda wake mwingi kujigunza na na ya kupiga hatua zaidi,
Na maskini anaweza kuua ili kuwa tajiri na hutumia mda wake mwingi kusengenya,kueneza chuki,Ubinafsi na Kuwaza Uwasherati.
Ukiona kijana anaamua kufundisha, kujifunza mambo mapya, ambaye anajaribu kujiboresha mara kwa mara, ujue kwamba yeye ni tajiri.
Ukiona kijana anafikiri kuwa tatizo ni serikali, na anayedhani kuwa matajiri wote ni wezi na anakosoa kila mara,kusengenya au kuwasema vibaya Viongozi wake ujue huyo ni masikini.
Tajiri wanaamini kwamba wanahitaji tu habari na mafunzo ili waweze kutoka, maskini wanafikiri kwamba lazima wengine wawape pesa ili watoke.
Samahani kwa kusema hivi, lakini wahalifu wengi ni watu masikini. Wakiwa mbele ya pesa wanapoteza akili ndio maana wanaiba, wanaua n.k... Kwao ni neema kwani hawajui wangewezaje kujipatia pesa..*inaendelea*
*... wewe ni tajiri au maskini?*
📚🖌
*streetlecture*
Comments
Post a Comment