HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI YATOA MIKOPO YA 10% SHILINGI MILIONI 141 KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE VIJANA NA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM


Na Bazil Mjungu Singida:
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida imetoa mikopo ya asilimia kumi (10%) kutoka kwenye mapato yake ya ndani ya Shilingi milioni miamoja arobaini na Moja (141) na Verehani tatu katika Vikundi kumi na mbili vya Wanawake, Vijana na watu wenye mahitaji Maalum.


Vikundi vilivyo nufaika ni Pamoja  na vya Wanawake ambavyo ni kikundi Cha Ushirika Cha Siuyu, Kikundi cha Jonelaa cha Siuyu, Kikundi cha Heshima Wanawake cha Ikungi, Tumaini Stara Cha Iyumbu, Kikundi cha Mshikamano cha Iyumbu, Kikundi cha Faraja cha Mgungira, Kikundi cha Igembensabo cha Ng'ongosoro, Kikundi cha Ipililo cha Ng'ongosoro sambamba na Vikundi vya Vijana ambavyo ni Kikundi cha Kidundu cha Kipunda, Kikundi cha Roho safi cha Iyumbu, Kikundi cha Be the Light cha Kipumbuiko, Kikundi cha Vijana Chapakazi cha Ikungi na Kikundi Cha Walemavu cha Kwajaa cha Matongo,


Aidha, Mikopo hii imetolewa Leo February 7 kutoka kwenye nusu ya kwanza ya Bajeti ya Mwaka 2022/2023 Kama mchango wa asilimia kumi ya makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri, 


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi Ndugu Justice Lawrence Kijazi Amesema Halmashauri inatekeleza sheria ya kutenga na kutoa Mikopo hiyo ya asilimia kumi ambapo katika mwaka huu wa fedha Halmashauri imefanikiwa kutoa Shilingi Milioni miamoja arobaini na Moja (141) na Verehani 3 katika Vikundi kumi na mbili vya wanufaika Pia Halmashauri kwa Miaka Mitano iliyopita imefanikiwa kutoa shilingi milioni mia sita (600) na fedha hizi zinazunguka kwa ajili ya kukopesha wanawake Vijana na watu wenye uhitaji maalumu Kijazi Aliongeza kuwa hatua hiii ni muendelezo wa kutoa mikopo kwa makundi katika Halmashauri ili kuyawezesha kiuchumi na itasaidia kupunguza umaskini na utegemezi. 


Nae Afisa Maendeleo wa ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Haika Masawe, amesema kuwa idara yake licha ya kusimamia mikopo inatoa pia elimu ya fedha kwa wanufaika wote na kusimamia urejeshwaji wa mikopo kwa wakati ili watu wengine wakopeshwe na kunufaika na mikopo inayotolewa na halmashauri.


Aidha, Mwenyekiti Wa huduma za jamii ndugu Misai ambae pia ni Diwani wa Kata ya Isuna (Ccm) Amewataka wanufaika kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyo kusudiwa na kuhakikisha kwamba mkopo huo ambao hauna riba wanaurejesha kwa wakati.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Ikungi Mhe. Ali Juma Mwanga ambae nae alihudhiria katika hafla hiyo ameipongeza halmashauri pamoja na Mkurugenzi kwa kutenga fedha hizo ambazo sitaenda kuchochea Maendelea kwenye maeneo mbalimbali kupotia Vikundi hivyo ambapo amevitaka kuhakikisha wanarejesha kwa wakati ili kuruhusu wengine kupewa Mikopo hiyo na wao kupewa kwa awamu zingine.

#bazotvnews
#bazotvonline


Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida