IKUNGI: DC MTATURU AMFUTIA MKATABA MASHANJALA AMBAYE NI MKANDARASI WA JENGO LA ZAHANATI MNYANGE KWA KULITELEKEZA KWA MIAKA 7.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu Ameagiza kusimamishwa kwa Mkataba baina ya Serikali ya Kijiji cha Mnyange na Mkandarasi Aliyejulikana kwa jina moja la MASHANJALA aliyekua akijenga Zahanati ya Kijiji aliyesababisha ujenzi kusimama kwa muda wa miaka saba (7).

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jirani na eneo la jengo hilo la Zahanati, DC Mtaturu amewataka Serikali ya Kijiji kuwa karibu na wananchi ili kushirikishana kutatua changamoto za maendeleo kwa pamoja, kwani kutowashirikisha wananchi ndiyo chanzo cha kupoteza uaminifu kwa viongozi wao.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu Amewataka Wananchi wa Kijiji cha Mnyange kuendelea kuwa na subira kwani Serikali inayo ongozwa na Rais wa Wanyonge Dkt John Pombe Magufuli aliahidi kuwatumikia wananchi wote kwa usawa bila ubaguzi na kuhakikisha zinajengwa Zahanati kila Kijiji Tanzania ili kuhakikisha kunatokomezwa kwa tatizo la kufariki kwa Mama na Mtoto na kutoa huduma kwa Wazee.

Ndugu wananchi wa Kijiji cha Mnyange najua mliamua kuchanga fedha zenu kwa ajili ya kujenga Zahanati yenu wenyewe, mkatafuta Mkandarasi wenyewe na akaanza kazi lakini hajaimaliza na ni kwa muda mrefu, lakini niwaambie tu huyo Mkandarasi sio mzuri kwani amewatamkia garama ambazo si halali kwa ujenzi huo wa kulifikisha jengo kwenye lenta, kwahiyo hafai na ninatangaza hapa mbele yenu Kusitisha mkataba huo na badala yake mtafute fundi mwingine ili aweze kumalizia kazi iliyobaki.

Jengo la Zahanati ya Mnyange ambalo Mkandarasi MASHANJALA amelitelekeza kwa miaka saba (7).

Mifuko ya Saruji iliyoharibika baada ya kutelekezwa kwa muda wa Miaka  saba (7) na Mkandarasi MASHANJALA.

Aidha DC Mtaturu Amewashukuru wananchi wa Kijiji cha Mnyange na Viongozi wake kwa kuwa na utulivo na kutojichukulia Sheria mkononi na hatimaye sasa Mkandarasi amemsitishia mkataba, na amewataka wao sasa waendelee na ujenzi kwa kumtafuta Mkandarasi mwingine.

Pamoja na hilo DC Mtaturu amewahimiza wazazi kutoa huduma ya Lishe Shuleni, kwani mwanafunzi anatoka asubuhi hadi mchana bila kula,  kitendo ambacho kinapelekea mtoto kukaa na njaa kwa muda mrefu na badala yake akiwa darasani badala ya kusoma utakuta anafundishwa na haelewi anachofundishwa,

"Nafaka shuleni kwa ajili ya watoto wetu sio mchango, Bali ni kuhamishia chakula kidogo tu ambacho kwa mwaka mzima imekadiriwa kuwa ni kilo 10 tu za nafaka ambazo zitamfanya mwanafunzi kuwa na mafanikio mema katika Masomo yake"

DC Mtaturu akiongea na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mnyange akiwataka wawafikishie wazazi ujumbe wa Lishe Shuleni.

MWISHO.

@bazilmjungu#



Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida