IKUNGI: DC MTATURU ANAENDELEA NA ZIARA YA KUHAMASISHA WANANCHI KULIMA KILIMO BORA
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu Ameendelea na ziara yake katika Kijiji cha Matongo ya kuhamasisha wananchi kuandaa mashamba na Kulima Kilimo bora na chenye tija ili kuondokana na Kilimo cha mazoea ya kutumia Mbegu zisizo rasmi badala yake wanunue Mbegu na kuzipanda kama wataalam wa Kilimo wanavyo elekeza.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, amewapongeza wananchi wa Matongo kwa kuweza kulima na kupata chakula cha kutosheleza.
"Kwanza niwapongeze wananchi wa Matongo kwa kulima mazao ya chakula na kuweza kujitosheleza kwa eneo lenu hili, Pili niwashukuru kwa ushirikiano wenu mkubwa wa kuweza kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha maendeleo ya Kijiji chenu yanakuwepo"
Aidha DC Mtaturu ameagiza ma Afisa ugani wawe karibu na wananchi ili muse kujua mahitaji yao muhimu hasa kwa kipindi hiki cha kuandaa mashamba.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, Amewahamasisha wananchi kulima zao la Pamba kwani ni zao pekee linalo weza kustahimili ukame na linatoa mavuno mengi na soko lake ni la uhakika.
"Ndugu wananchi niwaambie kuhusu hiki Kilimo bora cha PAMBA, Pamba ikishaota tu basi we jua Mshiko Njenje, kwanini nasema hivi, Pamba ukipanda kwa kuzingatia Kilimo bora lazima upate zaidi ya kilo 500 katika ekar moja ama zaidi, kwahiyo niwaombe wananchi na Taasisi zote za Serikali na binafsi kutenga ekar moja tu kwa ajili ya Kulima PAMBA kwani kwanza mbegu tunakopeshwa na madawa ya kupulizia ama ya kuulia wadudu tunapewa bure lakini si ivo tu bei yake ni nzuri na soko lake ni la uhakika.
DC Mtaturu akaongeza kwa kusema kwakua kampuni ya Biosustain inayojishughulisha na Pamba ndiyo inayotoa mbegu na dawa za kuulia wadudu nao watakua karibu kuhakikisha wanamsaidia mkulima kuona shamba lake linaendelea vizuri.
MWISHO.
@bazotvnews
Comments
Post a Comment