SINGIDA: MKUU WA MKOA WA SINGIDA AKAGUA UJENZI WA DARAJA MINYUGHE IKUNGI

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amefanya ziara ya kukagua Daraja katika Kijiji cha Misake Kata ya Minyughe Wilayani Ikungi, ikiwa  ni kuhakikisha Fedha za Serikali zinatumika ipasavyo na si vinginevyo.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi. akitoa msisitizo kwa Injinia wa Tarura Mkoa na kumwambia asifikiri ni ngonjera yeye kuja kukagua Daraja hilo amemtaka kuhakikisha anasimamia ujenzi huo unakua imara na kumsimamia Mkandarasi kuhakikisha kazi inakua imara na salama wakati wote na kabla Daraja hilo kuanza kutumika atataka taarifa rasmi inayo onyesha utekelezaji wa kiwango cha hali ya juu.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akipokea maelezo kutoka kwa mkandarasi wa Kampuni ya Mcharo Group Company LTD Ndg Adam Ibrahim.

Mhe. Mkuu wa Mkoa naomba niseme na nitoe shukrani kwanza kwa Serikali inayo ongozwa na Kipenzi chetu Dkt. John Pombe Magufuli kwani amekua akifanya kazi kwa kujiamini na kutufanya sisi tunao aminiwa na watumishi wake tuwe na furaha na utekelezaji uliotukuka na uaminifu, Mhe. mkuu wa Mkoa naomba nikuahidi kwa niaba ya Kampuni ya Mcharo Group Company LTD kuwa kazi hii tutaimaliza vema na tutaikabidhi kwa muda uliopangwa.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akipokea maelezo kutoka kwa Injinia wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Haruna Mbagala akimhakikishia kuwa kazi inaendelea vizuri na kumtoa hofu kuwa kazi itamalizika na itakabidhiwa ikiwa iko salama kwa matumizi na kuleta tija kwa wananchi wa Minyughe na Tanzania kwa ujumla.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa kusimamia vema shughuli za Serikali na kuhakikisha wananchi wanafaidika na kuzirurahia kura zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Justice Lawrence Kijazi Akimshukuru Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Injinia kwa kusimamia vema Fedha za Serikali na Kuona kinacho fanyika kwa ufuatiliaji wa karibu, na kuifanya Halmashauri kutambua uthamani wa Fedha kwa matumizi bora ya utekelezaji na kuwafanya wananchi kuiamini Serikali yao.

"Napenda kusema na kuwahakikishia wananchi wa Ikungi kuwa Serikali inayo ongozwa na kipenzi cha Watanzania Dkt John Pombe Magufuli, Kiongozi anaye tetea wanyonge, anaendelea kukamilisha ahadi yake ikiwa ni pamoja na kujenga madaraja na barabara za Wilaya yetu ya Ikungi, Mhe. Mkuu wa Mkoa naomba kusema kuwa nitawasimamia kwa karibu wakandarasi hawa na watakabidhi kazi ikiwa salama kwa matumizi ya wananchi wetu.

Hili ndilo DARAJA kubwa lenye Upana wa Mita 6 na Uredu wa mita 41.

Picha ya Daraja la pili lililokaguliwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.


Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ikungi Ndg Justice Lawrence wakikagua Mradi wa Ujenzi wa Daraja.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wakandarasi waliopewa kazi na Serikali kufanya kazi kwa uaminifu na kuikamilisha kwa wakati.

Mkuu Huyo wa mkoa amewataka wananchi kuzitunza vema Barabara hizo zinazo tengenezwa na Serikali kwa garama kubwa na kuhakikisha wanatunza Mazingira na kuhakikisha wao wanalinda na kuzingatia sheria za nchi.

MWISHO.

@bazilmjungu#

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida