IKUNGI: DC MTATURU AFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA MGUNGIRA
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu amefunga mafunzo ya Mgambo Jeshi la Akiba katika Kata ya Mgungira wilayani Ikungi Singida Baada ya Jeshi hilo kufanya mafunzo kwa muda wa miezi minne. Katika Mafunzo hayo Askari wa Jeshi la akiba wamejifunza mbinu mbali mbali ikiwemo jinsi ya kuilinda Nchi yao na kufundishwa kuwa tayari wakati wowote kwa maafa na majanga mbalimbali.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu amewataka Askari wa Jeshi la akiba waliohitimu mafunzo hayo kuwa na umoja ili kuweza kujenga umoja wa Jeshi hilo:
"Mimi Kamanda wa Jeshi la Akiba wilaya ya Ikungi, nitahakikisha mnaunda Kikundi chenu cha kudumu ili tunapo hitaji kuwatumia katika shughuli za Serikali na za kijamii tuwe tunawapata kiurahisi kwani mtakua na uongozi na lazima mfungue akaunti benki kwa ajili ya mfuko wa Kikundi na Mimi kwenye Akaunti yenu nitawawekea Pedha ya kuanzia Tsh.1000,000/= Milioni moja ili mnapoanza shughuli zenu za ujasiriamali ziwasaidie kuweza kuendesha miradi yenu"
Aidha DC Mtaturu ameagiza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha inasimamia kusajiliwa kwa Kikundi hicho na kuwatambua kikamilifu Askari hao, wakati huohuo ameitaka Serikali ya Kijiji cha Mgungira kuwapatia Kikundi hicho Ekari 10 kwa ajili ya Kilimo ili waweze kujikimu kimaisha na kuwa mfano mzuri kwa jamii.
DC Mtaturu akipokea maelezo mafupi kutoka kwa Mkufunzi wa Jeshi la Akiba Emanuel Matunda.
DC Mtaturu Akikagua Gwaride la wahitimu wa Jeshi la Akiba Mgungira.
SSGT fortunatus Ndalama Mshauri wa Jeshi la Akiba wilaya Ikungi Akisimamia vema ukaguzi wa Gwaride.
DC Mtaturu Kulia na SSGT fortunatus Ndalama kushoto mbele ya Wahitimu wa Jeshi la Akiba.
Kamanda wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua Choo cha Shule ya Msingi Mgungira kilichojengwa na Askari wa Jeshi la Akiba waliohitimu.
Wahitimu wa Jeshi la Akiba Mgungira wakisiiiliza hotuba ya Kamanda wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu.
Askari wa Jeshi la Akiba waliohitimu mafunzo wakifurahia hotuba ya Kamanda wao wa Jeshi la Akiba Wilaya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, Baada ya kuwaahidi Kuwawekea Tsh 1000,000/= kwenye akaunti yao ya Kikundi Mara tu watakapo maliza usajili na kufungua Akaunti Benki.
DC Mtaturu alimalizia kwa kuwashukuru wananchi na viongozi wa Kata na Kijiji kwa ushirikiano walioutoa katika kambi ya Jeshi la Akiba ya muda kwa kipindi chote cha Mafunzo.
MWISHO.
@bazilmjungu#
safi sana
ReplyDelete