IKUNGI: DC MTATURU AHIMIZA LISHE MASHULENI IWE KIPAUMBELE KUMSAIDIA MWANAFUNZI.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. MIRAJI Jumanne Mtaturu Ameendelea na ziara yake ya kazi katika Kijiji cha Kinku Kata ya Mungaa akihamasisha wananchi Kuendelea kutoa huduma ya Lishe Mashuleni na Kujenga Zahanati katika Kila Kijiji.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu Katika ziara hiyo Amewahimiza Wazazi na Walezi kuwa wanahakikisha wanatoa huduma ya Chakula cha Mtoto Shuleni ili kumsaidia Mwanafunzi kufanya vizuri katika masomo.
"Ndugu wananchi niwaombe kwa dhati ya moyo wangu kabisa, watoto hawa ni wetu sote na hawa Watoto ni msaada kwetu hapo baadae, ili kumfanya mwanafunzi awe msaada kwetu ni lazima tuhakikishe anasoma akiwa hana njaa, tunapo acha kutoa huduma ya chakula Shuleni ni kumtesa mwanafunzi na mwisho wake hawezi kufanya vizuri katika masomo yake" lakini pia kiasi cha nafaka ni kilo 10 tu na hii sio mchango ni kuhamisha chakula cha mwanao anachokula akiwa nyumbani na kumsogezea Shuleni ili asipate tabu ya kukaa na njaa kwa muda mrefu na kumsababishia kutoelewa kabisa walimu wanao wafundisha.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu amewataka Wazazi kuhakikisha wanatokomeza swala la Mimba za Watoto mashuleni kwa kuwa karibu na Watoto wao na kuwapa nahitaji muhimu kwani huenda kupungukiwa kwao na mahitaji ikawa ndiyo chanzo cha kushawishiwa na kupata Mimba zisizo tarajiwa na kumkatisha Mtoto masomo yake.
Aidha Dc Mtaturu: Amewataka Walimu kuwa na ushirikiano na Wazazi ili kupata taarifa kamili za wanaowapa Mimba Wanafunzi na kuweza kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
DC Mtaturu Ametembelea eneo la kujenga Kituo cha Zahanati katika Kijiji cha Kinku na kutoa Tofali 300 kwa ajilia ya kuwaunga mkoni wananchi kwa kuanzisha mradi huo, wakati huohuo DC Mtaturu Amewaunga mkono Kijiji cha Kinku kwa kuwapatia Mbabati 20 ili kukamilisha Jengo la Ofisi ya Kijiji iliyokwama kwa muda mrefu.
Aidha DC Mtaturu amewataka wananchi kuhakikisha wanajitoa kwa hali na Mali ili kuweza kusimamisha Jengo hilo la Zahanati na Serikali itawaunga mkono kwani Halmashauri ya Ikungi ina kauli mbiu inayosema, UKITAKA KUSAFIRI KAA STENDI ikiwa na maana ya anayeanziasha jambo ndiye mwenye kuungwa mkono.
Wananchi wa Kijiji cha Kinku wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu akiwataka kuwatunza watoto wao ili kuepukana na Mimba za utotoni.
Mwisho DC Mtaturu amewashukuru wananchi kwa kuitikia wito wa Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli wa hapa kazi tu na kuanza kufyatua Matofali kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati.
MWISHO.
@bazotvnews
Comments
Post a Comment