MTATURU ACHANGIA VYEREHEANI 10 CHUO CHA KIISLAM - JIMBONI


Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu ameshiriki Sherehe za Maadhimisho ya kutimiza Mwaka Mmoja tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Kiislamu Cha (Almadrasatul Tah Dhiibul Islaamiyaa) kilichopo Kata ya Dung'unyi Wilayani Ikungi Singida Ambapo amewaomba Viongozi wa Dini kuhubiri Umoja na mshikamano.

Mbungehuyo baada ya kuwasili na kujionea Mazingira ya Wanafunzi wanayojifunzia alionyesha kufurahishwa na usimamizi wa Chuo hicho ambapo bila kumumunya maneno aliamua kutamka kuchangia Vyerehani 10 na Seti moja ya Ufundi Seremala ili kuwafanya Wanafunzi kusoma kwa vitendo na wakimaliza masomo yao wakawe mfano Bora kwa familia zao.

Akizungumza Katika Hafla hiyo ya Maadhisho Mhe. Mtaturu akasema

Nimefurahishwasana na mafunzo haya mnayofundishwa hapa Vijana,  na Ninataka niwaambieni kila mtu anapaswa kujua wakati upi wa kujiandaa kimasomo na wakati upi wa kupoteza, na Ninataka niwahimize wazazi na walezi wa hawa Wanafunzi hakuna kitu kizuri Kama kumuunga mkono mtoto ukigundua anapenda kusoma, Ni vema umpe slushirikiano kwa Sasa anapojiaikia kusoma kwani asipo soma baadae itaturudia wenyewe na Mtoto asiposoma na akajua chanzo ni wewe nakuambia atakurudia, atakurudia kwa namna gani, atakurudia kwa kuwa mzigo kwako, Lakini Pamoja na hayo na mimi Mwakilishi wenu nawaunga mkono kwa kuwachangia Cherehani 10 na Seti moja ya kujifunzia ufundi Seremala" Alisema Mtaturu.

Aidha Mhe. Mtaturu Amewaomba wananchi kuliombea Taifa ili kupata mvua na kuondokana na tishio la Ukame linaloendelea hasa Katika Mikoa ya Kanda ya Kati.


Mhe Mtaturu ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kata ya Dung’unyi kupata Shilingi Milioni 80 kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa katika Shule za Sekondari Dadu na Munkinya.

  • #bazotvnews
  • #bazotvonline
  • #mtaturujimboni


Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida