MAKAMANDA WA CHADEMA SINGIDA MASHARIKI WATIMKIA CCM

WANACHAMA wawili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wa Jimbo la Singida Mashariki Katika Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida wamekihama Chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na kile walichodai kukosekana kwa Demokrasia halisi wanayoinadi viongozi wakuu wa Chama hicho kila kukicha.

Wanachama hao ni aliyekuwa kampeni meneja wa kata ya Unyahati Philemon Ghula na aliyekuwa Mgombea Udiwani Kata ya Makiungu Julius Sunna.


Akizungumza mara baada ya uamuzi huo Ndugu Philemon Ghula amesema wamechukua uamuzi huo ili kuunga mkono juhudi za Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Miraji Mtaturu kwa kazi nzuri wanayoifanya.

"Rais Samia anafanya kazi nzuri sana inayoonekana na kila mmoja wetu, lakini pia Mbunge wetu Mhe. Mtaturu anatutumikia wananchi na tofauti ya yeye na mtangulizi wake inaonekana dhahiri, hivyo hatuoni sababu ya kutowaunga mkono," alisema Ghula.

Nae Sunna amesema amechukua uamuzi huo kutokana na kuchoshwa na ubabaishaji wa viongozi wao wasiotaka maendeleo ya wananchi.


Julius Sunna.

"Sisi tumeitumikia CHADEMA kwa miaka mingi tena kwa kujitolea lakini hawakutambua thamani na mchango wetu, "alisema Julius.

Mika Likapakapa.

Kwa upande Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa amewapongeza wanachama hao wapya na kuwakaribisha wakijenge chama na nchi ili kuchochea maendeleo ya wananchi.

#SingidaMashariki#MaendeleoYetu#KipaumbeleChetu#KaziIendelee#


Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida