TANZANIA: MBOWE KUENDELEA KUTESEKA GEREZANI NI UDHAIFU KWA UPINZANI


Na Kibona Dickson.

(Mchambuzi huru).


Mwenyekiti wa chadema taifa na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni yuko gerezani kwa siku kadhaa.Anaweza kuendelea kubakia huko mpaka mwakani kwa sababu tumesikia korti zinaenda likizo mpaka mwakani.Kuna walakini kama rufaa ya upinzani itasikilizwa na uamuzi kufanyika mapema.


Kwa kumtia Mbowe gerezani,watawala wana akili za kuchungulia ili kuona aina ya upinzani uliopo nchini  kwa sasa ili baadaye waweze kufanya Mambo yao bila kusikiliza kelele za chura.


Tukio la   Mbowe kuwekwa rumande ni litmus paper ya watawala.Wamesoma mchezo wa upinzani.Siku zimeenda bila joto la  kisiasa kupanda nchini.Mbowe kiongozi wa chama kikubwa anaendelea kuteseka gerezani.Wafuasi wa chama kikubwa hawana la  kufanya zaidi ya kuandika mtandaoni.Watawala wameshajua litmus paper yao inasomeka "upinzani ni dhaifu kwa sababu wafuasi wa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani hawana la  kufanya."


Yule mgombea urais mwenye mamilioni ya wafuasi kashapewa kejeli "nenda kawaambie wasipotii sheria wataishia gerezani".Watawala wamemweka kwenye viganja vyao.Anaendelea kujivunia sifa za kuitwa mstaraabu na mwenye hekima.Huenda anaandaliwa tuzo ya siasa za kistaarabu.


Ukiangalia upinzani wa baada ya uchaguzi wa 2010,uko tofauti na ule  wa baada ya uchaguzi wa 2015.


Baada ya uchaguzi wa 2010,nchi ilikuwa na upinzani unaosonga mbele kupambana bila kuogopa vitisho vya watawala.Aliyekuwa Mgombea  urais wa wakati ule(Dkt Slaa) alikuwa front line.


Maandamano ya tarehe 5  januari 2011,yaliwaingiza viongozi wakuu wa Upinzani kwenye kesi ya jinai  kama walionayo Kina Mbowe sasa.Katika maandamano yale Dkt Slaa aliongoza maandamano akiwa na kilema cha mkono.Ni kiongozi pekee aliendas kwenye maandamano na mkewe.


Kesi ya jinai  ilifunguliwa dhidi ya viongozi wakuu wa wapinzani kwa kufanya maandamano yasiyo na kibali;Katika waliofunguliwa kesi miongoni mwao  ni Mbowe,Slaa,Lissu,Lema,Hayati  Ndesamburo nk.Siku ile Mbowe hakuwa amekamatwa na kupelekwa mahakamani.


Baadaye,Walimkamatia Dar Es Salaam.Nilikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dare Es Salaam.Tulikuwa na umoja wa CHASO,tulihamasika kwenye makao makuu ya Chadema ili kufanya maandamano ya kushinikiza Mbowe aachiwe huru.Joto la siasa za maandamano lilipanda Mikoa mingi.


Mawakala wa serikali ikabidi wafanya mambo haraka kuhofia nchi kuingia kwenye gharama ya kuzuia machafuko.Mbowe alisafirishwa haraka kwa ndege hadi Arusha kupelekwa mahakamani.Asubuhi yake aliachiwa huru.


Kuachiwa huru haraka kwa Mbowe kulitokana aina ya upinzani ambao ulikuwepo miaka ile baada ya uchaguzi wa 2010.Vitisho vilikuwepo na hata kukatamatwa na kuwekwa ndani,watu walikuwa wanapoteza maisha.Haya hayakuwa  sababu ya kurudi nyuma.Wanachama walijengewa spirit ya ujasiri mkubwa.


Siasa za woga zimeanza baada ya uchaguzi wa 2015 na hasa baada ya Lowassa kuingia chadema.Vijana ambao walikuwa jasiri miaka ile,wamejengewa na kuhubiriwa woga.


Vijana na wanachama wengine walikuwa tayari kushiriki bila woga.Wamekatishwa tamaa na viongozi waandamizi wa chama.Inaaminika Lowassa alihusika kuhakikisha maandamano ya UKUTA hayafanyiki.Hili linaweza kuwa na ukweli.Haiwezekani kina Mbowe,Lissu,Lema,n.k wa mwaka 2010 wageuke ghafla namna hii.Lazima itakuwa influence ya mtuhumiwa mkuu wa ufisadi nchini.


Mbowe alijipa ujasiri hivyohivyo kujitokeza kuahirisha maandamano ya UKUTA Mara mbili mfululizo.


Tunaomjua Mbowe tangu mwanzo hakuwahi kuwa na tabia ya kuongoza chama kwa kuahirisha mipango iliyopitishwa na kamati kuu.Ziku zile 2011,yale maandamano yalipigwa maarufuku na Polisi,lakini Mbowe na wenzake walisonga mbele.


Baada ya kuzuiliwa kwa Mikutano na maandamano ya UKUTA,Vijana wa BAVICHA waliunda mshikamano wa kwenda kuzuia mikutano wa wa ccm Dodoma uliofanyika Juni 2017.


Mbowe ndiye aliyewakatisha tamaa vijana kwa kuzuia hamasa ya vijana kwenda Dodoma.Bila hata kufanya consultation na vijana Mbowe alijitokeza kwenye Vyombo vya habari na kusitisha harakati zao kibabe.Hapa inaaminika pia,katika uamuzi wa Mbowe kulikuwa na mkono wa Lowassa.


Kamanda wa anga aendesha ndege  kwa mtindo ambao unapendwa na watawala chini ya aliyekuwa mgombea urais ambaye anaogopa mapambano.


Kamanda wa anga amejenga na kuimarisha siasa za woga miongoni mwa  vijana kiasi kwamba hata baada ya kukamatwa na kutiwa kwake gerezani hakuna joto la  kisiasa.Vijana wako kimya,wako mitandaoni kulalamika.


Laiti angeongoza chama kwa kuzingatia siasa za kiharakati kama baada ya uchaguzi wa 2010,asingekaa gereza  hata kwa siku moja.


 *Tatizo kubwa ni chadema + Lowassa influence.* 


Mwanaharakati huru.

kibonadickson@gmail.com.

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida