IKUNGI: KAMATI YA SIASA MKOA WA SINGIDA YATINGA IKUNGI KUKAGUA MIRADI YENYE THAMANI YA 4.2 BILIONI.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida. Mhe. Juma Kilimba akiipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo ongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri aliyojionea mwenyewe katika Wilaya ya Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. MIRAJI Jumanne Mtaturu akiipongeza Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi mkoa kwa utayari wao wa kukijenga Chama na kuanza ziara ya kukagua miradi.
DC MTATURU Akitoa taarifa fupi kwa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida iliyo ongozwa na Mwenyekiti wa Chama Mhe. Juma Kilimba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Justice Lawrence Kijazi, akitoa taarifa ya Maendeleo ya Miradi na Shughuli za huduma kwa wananchi kwa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Mhe. Mika Likapakapa Akiwapongeza Kamati ya Siasa Mkoa kwa Singida kwa kuja kukagua Miradi.
Aidha Mhe. Likapakapa amewataka watumishi wa Serikali kuwa na nidhamu na Chama Cha Mapinduzi kwani mshahara wao unatoka huko na si vinginevyo, pia amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuwa na Uzalendo wa kukipenda Chama chao na kuipenda Nchi yao na kutokua na mitafaruku isiyo na mitazamo chanya.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Ndg Solomon Kasaba akitoa neno kwa Halmashauri:-
Sisi kilicho tuleta ni kukagua DUKA letu kutaka kujua je bidhaa zetu zipo?..
Akimaanisha Chama Cha Mapinduzi Kimewekeza watumishi na Rasilimali mbalimbali kwa wananchi hivo wamekuja kuona zipo?.
Miradi iliyo kaguliwa:
1. Nyumba atakayo ishi Mkuu wa Wilaya.
2. Nyumba atakayo ishi Katibu Tawala Wilaya.
3. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
4. Maejengo ya Halmashauri ya Wilaya Ikungi.
5. Zahanati ya Kijiji cha Mang'onyi.
6. Nyumba ya Mganga Mang'onyi.
7. Kituo cha Polisi Mang'onyi.
8. Nyumba za walimu Lighwa Sekondari.
9. Kiwanda cha Chaki Mwisi.
10. Kituo cha Afya Ihanja.
Mhe. Msita MNEC Singida amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Mtaturu kwa kazi nzuri inayo oneka na kumuahidi kumpa ushirikiano pale inapolazimu.
Aidha Mnec Msita. amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kuongeza juhudi kwani juhudi sake zimeonekana na kumtaka kuendelea na ushirikiano huo ili kuifanya Serikali kujidhatiti katika kuwafikishia wananchi mahitaji yao muhimu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida. Mhe. Juma Kilimba alimaliza kwa kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi na Watumishi kwa ushirikiano walio uonyesha kwani Miradi waliyo ipitia Hakuna yenye kasoro ingawa mapungifu madogo sana na huwa hayakosekani kwa kila mwanadamu.
Aidha Mwenyekiti wa Chama Mhe. Juma Kilimba amewataka Chama Wilaya kuwa Karibu na wananchi na Serikali ili kuongeza uaminifu wa dhati na utekelezaji mathubuti.
MWISHO
@bazilmjungu#
Comments
Post a Comment