IKUNGI: DC MTATURU AAGIZA KUUNDWA KAMATI YA KURATIBU MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI IKUNGI


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, Ameagiza kuanzishwa kwa Kamati ya Kuratibu na kusaidia Vyama vya watu wenye ulemavu Wilayani Ikungi.

Akiongea katika Mkutano huo Bi. Ummy Nderiananga Mwenyekiti wa SHIVYAWATA  Taifa, amesema umefika muda sasa wa kujua umuhimu wa kuwapa kipaumbele na kuwajumuisha ipasavyo  watu wenye Ulemavu  wa aina zote ili kutambulika na wao kujitambua kuwa taifa linawategemea.Ametoa Mfano wa Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli alivyowajumuisha watu wenye ulemavu Kwa kuwateua kushika nafasi mbalimbali za maamuzi Serikalini.Huo ni Mfano chanya unaopaswa kuigwa na Viongozi wengine wa serikali katika maeneo yao mbalimbali  ya kazi.

Akisoma taarifa fupi kutoka Idara ya Elimu, Elimu Maalum, Afisa Elimu, Elimu Maalum Ndg. Peter Ngatunga, taarifa iliyo onyesha Chama Cha watu wenye Ulemavu kutopata ushirikiano kikamilifu kutokana na kutokuwepo wafuatiliaji wa karibu (Kamati) inayoweza kutambua kwa urahisi mahitaji ya Walemavu Na kumfanya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Mtaturu kutoa tamko hilo la kuundwa kamati.

Dc Mtaturu, Akiongea katika mkutano huo wa pamoja uliohusisha viongozi wa Chama Cha watu wenye Ulemavu Shivyawata, Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Wadau mbalimbali ameagiza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Ikungi, kuhakikisha Kamati hiyo inaundwa haraka iwezekanavyo ili kusaidia kupata takwimu halali ya watu wenye Ulemavu na kuweza kugundua walemavu walipo hasa wale ambao familia zao hazipendi wajulikane.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu (Kulia) pichani, amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi (Kushoto) pichani, Ndg Justice Lawrence Kijazi kwa ushirikiano anao utoa kwa vikundi vya watu wenye Ulemavu hususa ni ile asilimia 2 (2%) ya mikopo itokanayo na Mapato ya ndani ya Halmashauri na kuwafanya watu wenye Ulemavu kuendelea kuiamini Serikali inayo ongozwa na Rais wa wanyonge Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.

DC Mtaturu, amewataka Viongozi wa Chama Cha watu wenye Ulemavu Shivyawata Mkoa wa Singida, kuandaa mpango kazi ili kuwepo na njia ya kuonyesha tatizo lililopo ili kuepusha ulalamishi kwa walemavu wachache ambao hawafikiwi na Chama ama Serikali kwa muda muafaka mahali walipo.

Aidha, DC Mtaturu, Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, kwa kuwajali walemavu Nchi nzima na kwa kuonyesha Upendo mkubwa na wa dhati kwao hata kuendelea kuwateua kuwa Viongozi wa Kitaifa na kuwafanya kuwatetea wanyonge hususa ni Walemavu na amempongeza Raid kwa kuwatengea 2% ya pato la Ndani.

DC Mtaturu amewataka wananchi kuendelea kuwa na upendo na watu wenye Ulemavu na kuto wabagua ili kuwapa furaha nao kujivunia kuwepo Tanzania.

Ndg. Justice Lawrence Kijazi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, kwa kasi ya maendeleo inayo onekana na kuzidi kuwafurahisha Watanzania wanao muelewa na kutambua utendaji kazi wake hususa ni kwa 2% ya mikopo kwa watu wenye Ulemavu, Aidha amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu kwa kuthubutu na kwa utayari wa Kuunda Kamati itakayo hudumia watu wenye Ulemavu.

MWISHO.


@bazilmjungu#


Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida