IKUNGI: KIKUNDI CHA VUMILIA VIKOBA MAKIUNGU WASHEREHEKEA KUMALIZA MZUNGUKO WA AWAMU YA TATU (3)


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, Ameshiriki Sherehe ya Kumaliza mzunguko wa awamu ya  Tatu (3) wa Kikundi cha Vumilia VIKOBA Makiungu mzunguko ulioonyesha kuwa na faida kubwa kuliko mizunguko miwili (2) iliyopita.

DC MTATURU amekipongeza kikundi hicho kwakua na Upendo mkubwa, Umoja na kuwa na Uongozi uliotukuka ambao umekifanya Kikundi hicho kuwa na uchumi mzuri uliopelekea kujikomboa na kujitosheleza katika kusaidia familia zao, Pia Dc Mtaturu, amewataka kuanzisha Mradi kiwanda Kidogo ili kuweza kuongeza kipato kwa wanakikundi na Kuongeza huduma kwa jamii jambo ambalo litawafanya wasiopenda kujiunga na vikundi wahamasike zaidi.

Aidha, Dc Mataturu amewataka wanakikundi hao kujiunga na Bima za afya ili kuepuka garama zinazo jitokeza pale mtu anapo ugua gafla, kadhalika Dc Mtaturu amewaomba wasiwe na ubinafsi ili vikundi vingine vidogovidogo viweze kuja kukopa katika kikundi chao na Uchumi wao utakua umekua na kuimarika zaidi.

Mhe. Miraji Mtaturu Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Amempongeza Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli Rais Mzalendo na Nchi yake kwa kuwaandalia wafanyabiashara wadogo wadogo  Vitambulisho na lengo lake ikiwa ni kuwainua kiuchumi.
Akihutubia wanakikundi hao amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kupeleka wataalam kufuatilia Kikundi hicho ili kujua uwezo walio nao kifedha ili waweza kufungua Benki yao wenyewe  Na ameagiza mkurugenzi kuhakikisha vikundi vyote vilivyopo wilayani vinakua na usajili wa kudumu ili kuweza kujipatia mikopo na kuaminika katika taasisi za Fedha.
Pia DC MTATURU amemwagiza Mwenyekiti wa Kijiji kuwapa kiwanja cha kujenga Ofisi yao Mara moja ili kuweza kuanzisha ujenzi wao haraka iwezekanavyo na kuwaahidi kuwapatia Mabati yatakayo hitajika kwenye jengo hilo na Kuwatunishia mfuko wao kwa Shilingi Milioni moja (1,000,000/= na amewapatia Mizinga 10 ya nyuki, kuahidi kuwalete elimu ya ujasiliamali lakini amewataka kujenga jengo lenye kukidhi mahitaji ya Benki.

Mhe. Yustina Raphael Mbugha, Mwenyekiti wa Kikundi cha Vumilia Vikoba Makiungu. akimshukuru Mhe. Miraji Mtaturu Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kwa kuwa na  ukaribu mkubwa na Vikundi na sio kuwa karibu tu bali kwa kuvisaidia na kwa kuviunga mkono ikiwa ni sambamba na kuhamasisha Maendeleo pia. Akizungumza kwa niaba ya Wanakikundia na amepongeza hilo kwa msisitizo mkubwa.

Bi Zainabu Hassan Ntui (pichani) Kushoto na Bi. Fortunata Petro Kisema (Kulia) pichani Katibu wa Kikundi akisoma taarifa fupi kwa mgeni Rasmi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu  na kufafanua tangu kuanzisha kwa Kundi hilo na kuweza kufanikisha kuwa na hisa yenye thamani ya Shilingi Milioni Themanini na tano laki mbili na sabini na name elfu. Tsh. 85,278,000/= kwa awamu hii ya Tatu, akisoma taatifa hiyo iliyo onyesha mafanikio na changamoto mbalimbali na kumkabidhi mgeni rasmi kwa hayua zaidi.

Moja ya Mwanakikundi (Kulia) Pichani akipokea Faida ya mgao wa Kikundi

Picha ya Wanakikundi wakipongezana.

Bi. Yustina Raphael Mbugha, Mwenyekiti wa Kikundi akishukuru kwa niaba ya Wanakikundi.

Mhe. Heken Petro Ayubu Diwani Viti Maalum Mungaa, akipokea moja ya faida za Vikoba.

Wanakikundi wakiwa kwenye furaha isiyo kifani na kupongezana.




Picha za pamoja Viongozi wa Kikundi, Uongozi wa Kata, Kijiji na Mhe.Miraji Jumanne Mtaturu Mkuu wa Wilaya Ikungi.

MWISHO.

@Bazilmjungu.

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida