IKUNGI: KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA WILAYA (DCC) CHA AZIMIA KUTOKOMEZA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI
Kamati
ya ushauri ya Wilaya DCC Ikungi ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu, ambaye ni Mkuu wa wilaya Ikungi , na Katibu wa kikao
Ndg Justice Lawrence Kijazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wilaya ya Ikungi.
Kamati
hii imekaa kwa mara ya kwanza tangu Halmashauri hiyo kuanzishwa Mwaka 2013 ambapo imejadili mambo mbalimbali ya
maendeleo.
Katika kikao hicho Mada zilizo pamba moto ndani ya ukumbi zilikua kama Maswala
ya kilimo bora chenye kuzingatia maelekezo ya wataalamu ili kuleta tija.
Usimamizi
wa Utawala bora. Kujitambua kama Mtumishi wa serikali na mwananchi kutambua
wajibu wake.
Kusimamia
Sheria na kutekeleza maagizo ya Serikali.
Uhaba
wa Madawati katika shule zote za Msingi na Sekondari.
Vifo vya Mama na
Mtoto, Ujenzi wa Zahanati na Vituo vya
Afya pamoja na Utokomezaji wa Mimba na Ndoa za utotoni.
Baada mjadala kuendelea kulijitokeza kauli zilizo onyesha dhahiri kua kuna viongozi wanaozuia wananchi kushiriki katika kazi za maendeleo kitendo kilicho pelekea Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. MIRAJI JUMANNE MTATURU Kumwagiza Mkuu wa Polisi wa wilaya kuwasaka na kuwakamata
viongozi wa kata ya MUNGAA na MAKIUNGU ambao wanatuhumiwa kuwakataza wananchi
wasichangie katika shughuli za maendeleo ikiwemo utengenezaji wa madawati
kwa ajili ya wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza hapo mwakani.
Mkuu
huyo wa wilaya ametoa kauli hiyo katika kikao cha Ushauri cha Wilaya hiyo mjini
Ikungi na kusisitiza kuwa kamwe Serikali haitamvumilia mtu au kikundi cha
wanasiasa ambao watakataza wananchi kuchangia shughuli za maendeleo ikiwemo nguvu
kazi kwani kufanya hivyo ni kurudisha nyuma shughuli za maendeleo za wananchi.
Aidha Katika
kikao hicho cha kujadili shughuli za maendeleo, Mkuu wa wilaya ya IKUNGI pia
ameiagiza watendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa katika wilaya
hiyo -TAKUKURU - kwenda kijiji cha MGUNGIRA kuchunguza uwepo wa vitendo vya
rushwa vinavyofanywa na kikundi cha watu wakidaiwa kushirikiana na Polisi kwa
kubambikizia watu kesi.
Kikao
cha Kamati ya Ushauri cha Halmashauri ya Wilaya ya IKUNGI kinafanyika mara ya
kwanza tangu halmashauri hiyo ianzishwe mwaka 2013.
MWISHO.
@bazilmjungu#
Comments
Post a Comment