DODOMA: VYAMA KUMI VYA UPINZANI VYATOA TAMKO KALI KUUNGA MKONO MABADILIKO SHERIA YA VYAMA VYA SIASA, VYASEMA RAIS NI JEMBE. AUNGWE MKONO.

Tamko la vyama vya siasa 10 limetolewa Dodoma kupiga matamko ambayo yamekuwa yakitolewa na Chadema na washirika wao kupinga Mabadiliko ya Vyama vya Siasa pamoja na Juhudi anazofanya Mhe Rais Dr John Pombe Magufuli.

Leo Jijini Dodoma limetolewa tamko linalopinga siasa chafu ambazo zimekuwa zikifanywa na Chadema pamoja na washirika wao kupinga juhudi na Kazi nzuri anazozifanya Mh Rais. Aidha tamko hilo linapinga upotoshaji unaofanywa  na baadhi ya vyama siasa dhidi ya Mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa. Tamko hilo limetolewa na Vyama kumi na moja ambavyo ni CUF,TLP,ADC,DP,NRA,AAFP,UMD,SAU UDP,na DEMOKRASIA MAKINI. Vyama hivyo vimeeleza kuwa vinasikitishwa na namna Mataifa ya Kigeni yanavyotoa fedha kudhamini mambo yanayolenga kuchafua taswira ya Taifa kupitia baadhi ya vyama vya Upinzani kama CUF SEIF na CHADEMA lengo likiwa kuichafua serikali ya Mhe Rais Magufuli anayepambana kuleta maendeleo. Imeelezwa kuwa wanayo taarifa kuwa mikataba ya madini iliyobadilishwa na Serikali na kuanza kuwanufaisha wazawa imewachukiza sana wazungu hivyo wameanza kuitumia CHADEMA kutaka kuikwamisha Serikali. Wamehoji fedha zilizotumiwa na Maalim Seif kufanya kikao cha siku tatu katika hotel ya kitalii kwa dola 450 zilitoka wapi kama siyo fedha za mabeberu wanowatuma. Kuhusuu kazi za Mhe Rais Magufuli wamefurahishwa na utendaji wake na wamesema wao binafsi watahakikisha wanamsaidia katika kumtetea na kumsemea katika kutimiza malengo yake kwa Taifa. Wamesema hawako tayari kuona Taifa linaingia kwenye machafuko kupitia tamaa za baadhi ya wanasiasa wanaojari matumbo yao tu. Katika kueleza hayo Msemaji wa CUF ABDUL KAMBAYA pamoja na Mkiti wa TLP wameyakemea mataifa ya kigeni kuacha kutngeneza chokochoko za kuivuruga amani ya nchi pamoja na kuacha kuamini propaganda za Chadema,ACT na NCCR MAGEUZI kwakuwa vyam hivyo vimekuwa na tamaa pamoja na uongozi mbaya katika vyama vyao jambo linalopelekea baadhi ya watu wachache kujinufaisha na misaada pamoja na ruzuku inayotolewa na serikali bila kunufaisha wanachama wengine hasa ngazi ya chini. Vyama hivyo vimemuomba Rais MAGUFULI kutengeneza utaratibu wa kuvipa ruzuku kuliko hao anaowapa ruzuku lakini bado wanaendelea kutumiwa na mabepari na watu wasioitakia mema Tanzania. Vyama hivyo vimehitimisha kwa kuweka msimamo wa kuiunga mkono Serikali na kuisaidia kwa kila hali kuhakikisha Mhe Rais anatimiza majuku yake kwa amani na Utulivu.

Dodoma.

@Vyama10.

Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida