SINGIDA: SERIKALI YATOA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) 2016-2018

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu. Akisoma taarifa ya utekelezaji ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa Singida Dr. Rehema Chimbi.

Kaimu huyo wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, Akisoma taarifa hiyo kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa Singida Dr. Rehema Chimbi, Ameelezea kwa undani Vitu vilivyo tekelezwa na Serikali ya Mkoa katika kutimiza wajibu wake kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Singida.

Akiwasilisha taarifa kwa niaba ya mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu  mbele ya Kamati ya Siasa ya Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Singida. amesema kwa kipindi cha miaka miwili mwaka 2016-2018 Ilani imetekelezwa vizuri kwenye sekta za Elimu, Afya, Maji, Miundombinu na Ulinzi na Usalama.

Aidha. Amempongeza Rais mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa maelekezo yake na kuleta fedha za miradi ya maendeleo iliyosababisha kutekeleza miradi yote ikiwemo vituo vya afya 10 vinavyoendelea kujengwa kwenye halmashauri zote za mkoa wa Singida kwa gharama ya shilingi bilioni 4.5.

"Tunamshukuru sana Rais wetu Mhe. John Pombe Magufuli kwa kutuletea pia kiasi cha shilingi bilioni 3.7 kwa ajili ya mpango wa Elimu bure kwa shule za msingi na shilingi bilioni 3.1 kwa shule za Sekondari zilizosaidia sana kuongeza uandikishaji wa wanafunzi kwenye shule zote za Mkoa wa Singida, "alisema mkuu huyo.


Amewahakikishia kuwa serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi na Kukihakikishia chama kuwa Serikali ya Mkoa itazidi kuwa karibu na Chama ili kutekeleza Ilani kikamilifu.


Comments

Popular posts from this blog

WASIFU BINAFSI JINA KAMILI: REHEMA SOMBI OMARY

IJUE FAIDA YA MSTARI WA IKWETA KUWA KARIBU NA NCHI YAKO

DC MTATURU Azindua Jengo la kituo cha huduma ya Mama na Mtoto Matare Ikungi Singida